Habari za Punde

Mahafali ya Kwanza ya Zanzibar School of Heath.

Brass band ya Chuo cha Mafunzo Zanzibar ikiongoza Maandamano maalum ya sherehe za Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Afya Zanzibar wakiingia katika viwanja vya sherehe. 
Wahitimu wakiingia katika Viwanja vya sherehe kwa maandamano maalum yalioandaliwa kwa sherehe hiyo yaliokuwa yakiongozwa na bendi ya Mafunzo.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Fatma Ferej akiwahutubia  Wahitimu hao wakati wa mahafali yao ya kwanza yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Shaa Mombasa Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Afya Zanzibar kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Iringa, Mhe Ali Saleh, akizungumza wakati wa mahafali hayo ya kwanza kwa Chuo hicho tangu kuazishwa kwa kutoa Elimu ya Afya.  

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Fatma Ferej, akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora Taaluma Yussuf Ali Nassor.
 Wahitimu wakifuatilia hutuba ya Mgeni rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Ferej.
 Wahitimu wa Chuo cha Afya Zanzibar wakimsikiliza Mgeni Rasmin wa Mahafali hayo ya Kwanza kwa Chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Shaa Mombasa kwa Mchina. 
Wazazi wa Wahitimu wa Chuo cha Afya Zanzibar wakifuatilia mahafali hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya sekondari ya Shaa,


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.