Na
Mwantanga Ame
WAJUMBE
wa Kamati 12 za bunge maalum za katiba wanatarajiwa kutangazwa leo.
Mwenyekiti
wa bunge hilo, Samuel Sitta, anatarajiwa
kutangaza kamati hizo ikiwa ni sehemu ya kazi zilizopangwa kutekelezwa baada ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kulizindua rasmi
bunge hilo .
Kabla ya kuifanya kazi hiyo, Sitta anatarajiwa kuendelea kuwaapisha wajumbe
wengine ambao bado walikuwa hawajaapishwa.
Uundwaji
wa kamati hizo ni sehemu ya utekelezaji wa kanuni za bunge hilo
amabalo lilipendekeza kuundwa kwa kamati 12 ambazo zitatumika kupitia rasimu
hiyo na baada ya kukamili kuwasilisha mapendekezo yao .
Wakati hatua hizo zikiendelea vyombo vya
habari havitaruhusiwa kuingia katika kamati hizo wakati wajumbe wakiendelea na
mjadala wao, na badala yake vitalazimika kupata taarifa hizo baada ya
kumalizika kupitia Mwenyekiti wake.
No comments:
Post a Comment