Na Joseph
Ngilisho, ARUMERU
KATIKA
hali isiyo ya kawaida Madiwani wa CCM katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani
wa Arusha wametishia kujiuzulu pamoja na kukusanya kadi zote za chama kutoka
kwa wananchi na kuongoza nao kwenda kuchukua
ardhi yao aliyokabidhiwa
mwekezaji iwapo serikali haitatoa tamko.
Walitoa
onyo hilo katika baraza la madiwani lililofanyika halmashauri hiyo ambapo, ajenda
ya migogoro ya ardhi ilifanya baraza hilo
kujikuta likitoa tamko na vitisho vikubwa kwa watumishi wa halmashauri hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya madiwani wenzake, diwani wa kata ya Maroroni, Mwanaidi Kimu, alisema
wamechoshwa kila siku kujadili ajenda za migogoro ya ardhi lakini hakuna
utendaji wowote na badala yake wanabaki wakiwa na kumbukumbu ya vikao katika
vichwa vyao hali ambayo kwa sasa imefika mwisho.
Akitolea
mfano moja ya shamba lenye migogoro, alisema ni shamba la Madira lililopo
maeneo ya Seela Singisi ambalo ni mali ya halmasahuri hiyo lakini kwa
sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa na baadhi ya viongozi wanaodai ni lao.
Akizungumza
kwa niaba ya madiwani wanaume,Wilson Nyitti, alisema hali hiyo imesababisha
kila wanapopita wakiwa wanazomewe na wananchi kwa kuwa wanafikiri wao
wananufaika na migogoro hiyo.
Mwenyekiti
wa halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola, alisema tamko hilo la kutaka kujiuzulu kwa madiwani wote 23
lipo sawa kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na viongozi wasio
waadilifu.
Akizungumzia shamba hilo la Madira alisema, Rais
Kikwete tayari ameshatoa ardhi hiyo yenye hekari 360 lakini bado hawajaweza
kulitumia kutokana na vitisho wanavyopewa
No comments:
Post a Comment