Na Mwandishi
wetu
MWANASIASA
mkongwe, Kingunge Ngombalemwiru, ameendeleza shutuma kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akisema Tume yake haikufanya utafiti
wa kina wakati ilipokusanya maoni kuhusu muundano wa Muungano wa serikali tatu.
Akizungumza
katika semina kwa wanahabari jana, Kingunge alisema, alisema Tume haikuakisi
mazingira ya uchumi wa Tanzania
na umuhimu wa Muungano uliopo sasa.
Alisema
ya kazi nzuri iliyofanywa na Warioba na jopo lake la wataalamu, lakini kazi
waliyoifanya ina upungufu mkubwa huku akitilia mkazo Muungano wa sasa wa
serikali mbili umesaidia kujenga umoja wa kitaifa Tanzania
na Tanzania
kuwa nchi ya mfano Afrika.
Alisema
Muungano uliopendekezwa na Tume utajenga matabaka ingawa unawafurahisha watu
wanaopenda madaraka.
Hata
hivyo, alionya kwamba hazi kubwa iko mbele kupata katiba bora itakayokubalika
na makundi yote, ikiwemo kuhakikisha hazi za makundi mbalimbali wakiwemo
wakulima, wafugaji na jamii Wahazabe ambao alisema kama hawatakikishiwa maslahi
yao ndani ya
katiba watatoweka.
Alisema
wao wakati wanapigania uhuru waliweka uzalendo mbele badala ya kugombania vyeo,
lakini hali hiyo ilibadilika baada ya uhuru na Mapinduzi, ambapo sasa wanasiasa
wapo kwa ajili ya kupigania maslahi yao
binafsi.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ali, licha ya kutangaza kuwa ni muumini wa muungano
wa serikali mbili, aliwataka wajumbe wa bunge la katiba kuondoa msuguano uliopo
ili Watanzania wapate katiba bora.
Aliwashauri
wajumbe kutumia hotuba ya Jaji Joseph Warioba, hotuba ya Rais Kikwete pamoja na
sheria nyengine kama miongozo muhimu
watakapojadili rasimu ya katiba.
Aidha,
aliwasihi wanahabari wanaoripoti bunge la katiba kuhakikisha makundi yote
yanayounda bunge hilo
yanapewa nafasi sawa badala ya kuripoti misimamo ya makundi fulani pekee.
“Mkianza
kuchagua kuwa hoja hii ina nguvu zaidi kuliko ile mtawapotosha wananchi,”
alisema.
Dk.
Ayoub Rioba, mtaalamu wa masuala ya habari na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , aliwasihi wanahabari kuripoti sawa yale
yanayotokea katika ukumbi wa bunge hilo .
Hata
hivyo, baadhi ya wanahabari walionesha hofu na wawasilishaji wa mada kuzungumzia zaidi masuala ya siasa na
mfumo wa serikali badala ya kuwaelimisha waandishi umhimu wa kuripoti masuala
ya bunge.
Walisema
walitarajia waandaaji wa mkutano huo wangewatafuta watoa mada walio huru ambao
hawaungi mkono mifumo yoyote ya serikali tofauti na mmoja ya wasiliajaji
(Bashiru Ali) ambae ameonesha msimamo wa kuunga mkono serikali mbili wakati
hapo si pahala pake.
kingunge kaa chonjo umkumbuke mola kwa wingi kwani muda ulionao kukutana nae sio mwingi, kama huu muungano ni mfano hapa afrika ni nchi gani zimetuiga? mbona tumeona sudani ikimeguka, ethiopia ikimeguka , jambo zuri huigwa na wengi , nani wametuiga kufanya muungano? msidanganye watu hapa , kakojoeni mkalale
ReplyDelete