Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif amewasili Mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Katka uwanja wa ndege wa Dodoma, Maalim Seif amepokelewa na viongozi wa Mkoa huo pamoja na Wabunge, Wawakilishi na viongozi mbali mbali wa CUF.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mbunge wa Mji Mkongwe Mhe. Ibrahim Sanya, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma. (Picha na Salmin Said, OMKR)
maalim seif huko tunataka uhuru wa zanzibar tu , usije kukubaliana na akina kikwete wala nani ,
ReplyDeleteAnanym, 1 bora wakumbushwe hawa watu...Ndani ya Bunge maalim ni mgeni wa kualikwa tu, sidhani kama atazungumza... Hata hivyo hiyo ni geresha ya Watanganyika kuona kwamba Ubatizo mpya wa Muungano umewahusisha kikamilifu Wapinzani...
ReplyDeleteWito wangu kwa Wabunge kutoka Zanzibar na Wawakilishi wetu kuwa macho na Na Watanganyika ambao wako mbioni kutaka kuitawala Zanzibar kimabavu kama vile Urisi ilivofanya kwa Crimia.. Nasikia baadhi ya CCM wahafidhuna wanataka katiba ya Zanzibar iliosema kwamba zanzibar ni nchi ifutwe na isisomeke hivo..... jamani huo si ndioujinga wa mwishooo? alimuradi wao wanapandishwa vyeo na Watanganyika wako tayari kuuza kila kila kitu...
uhuru wa znz, haupatikani, dodoma, utapatikana siku waznz, wenye watakapo amua, hivisasa bada tunahitaji kutawaliwa na ndugu zetu wa kitanganyi, hii imemeonesha wakati wa kutoa manoni, hatukujitambua, sembuse hivi sasa na serekali inayo aminiwa imeshindwa kutoa msimamo juu ya mabadiliko ya katiba
ReplyDelete