TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
12th
APRILI, 2014.
Wajumbe wa Baraza JUHIMKO,
Msimamizi Mkuu wa Jumuiya ya ACRA Nchini Tz,
Meneja wa Mradi,
Wanachama wa JUHIMKO,
Wageni Waalikwa,
Ndugu waandishi wa habari,
Mabibi na Mabwana
Assalaam
Alaykum,
JINA LA MRADI: Uhifadhi
wa Urithi wa Zanzibar
na Kutengeneza ajira. (Zanzibar
Built Heritage for job creation)
MUOMBAJI WA MRADI: ACRA
WASHIRIKA WA MRADI: ZSTHS (JUHIMKO), ACRA & AGSS.
ENEO LA MRADI: ZANZIBAR – TANZANIA .
MUDA: MIAKA MITATU.
GHARAMA ZA MRADI: EURO 1,200,000/=
LENGO LA MRADI: Mradi huu una lengo la
kuhifadhi, kutunza na kuutangaza urithi wa kiutamaduni uliopo Zanzibar na kuifanya sekta hii kuchangia
ukuwaji wa uchumi wa Nchi.
WALENGWA WA MRADI: Jumla ya watu wapatao
15,922 watafaidika na Mradi huu, wakiwemo mafundi ujenzi/waashi 400, watu wasio
na ujuzi 75, wajasiria mali katika sekta ya ujenzi na
ambao wamesajiliwa 22, wamiliki wa majengo ya umma na majengo binafsi
150, watembeza watalii wapatao 50, walimu wa
skuli za msingi na Sekondari 200, wanafunzi wa skuli za msingi na
sekondari wapatao 10,000, pamoja na wananchi wa kawaida 5,000 ambao watashirirki
katika mikutano na maonyesho mbali mbali.
SHUGHULI ZA MRADI: Mradi
huu utajumuisha shughuli zifuatazo;
1.
Kutoa mafunzo ya muda mfupi kuhusiana na matengenezo
ya majengo ya kiasili kwa watu wenye ujuzi na wale wasio na ujuzi.
2.
Mradi pia utasaidia kuanzishwa kwa maabara katika Chuo
Kikuu cha Taifa SUZA, ambapo maabara hiyo itasaidia kufanyia utafiti
unaohusiana na mali
ghafi zinazotumika kujenga majengo ya kihistoria.
3.
Mradi utasaidia kuandikwa kwa mtaala unaohusiana na
kuyafanyia matengenezo majengo ya kale ambapo mtaala huo utatumiwa na Chuo cha
Karume (Karume Institute of Science and Technology).
4.
Kuandaa na kufanya mikutano na wadau mbali mbali
kuzungumzia masuala ya urithi wa rasilimali za Kiutamaduni yakiwemo majengo ya
asili yaliyopo Zanzibar .
5.
Kutoa mafunzo
kuhusiana na masuala ya kufuata taratibu za uhifadhi wa majengo ya kihistoria
kwa wajasiriamali pamoja na watu wanaomiliki majengo binafsi na majengo ya
umma.
6.
Kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya urithi kwa
walimu, wanafunzi pamoja na jamii yote kwa jumla.
MATOKEO YA MRADI: Mara baada ya kukamilika
utekelezaji wa mradi huu, ni matarajio yetu kupata yafuatayo;
i.
Mradi utaweza kusaidia kuongeza ujuzi na ufanisi kwa
mafundi pamoja na watu wasio na ujuzi kwa kufanya kazi zao, huku wakizingatia
mbinu na taratibu sahihi za kiasili zinazotumika katika ujenzi na uhifadhi wa
majengo ya kihistoria.
ii.
Mradi utaweza kukisaidia Chuo Kikuu cha SUZA kwa
kuanzisha maabara ambayo itasaidia kufanya shughuli mbalil mbali za kiutafiti
unaohusiana na mali
ghafi zinazotumika kujenga majengo ya kiasili/kihistoria.
iii. Mradi
utaweza kusaidia Chu cha Karume (Karume
Institute of Science and Technology) kupata mtaala unaohusiana na kuyafanyia
matengenezo majengo ya kale.
iv. Pia mradi
utaweza kuwajengea uwezo wadau mbalil mbali katika sekta ya utalii wakiwemo watembezaji
watalii, hii itapelekea kutoa taarifa sahihi kwa wageni na wenyeji
zinazohusiana na historia pamoja na urithi tulionao.
v.
Vile vile mradi utasaidia sana kuwajengea uwezo na
uelewa wa kina kwa walimu, wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla kuhusiana na
historian a urithi uliopo katika Nchi yao.
NAFASI YA JUMUIYA YA HIFADHI MJI MKONGWE KATAIKA UTEKELEZAJI WA MRADI:
Kimsingi Jumuiya ya
Hifadhi Mji Mkongwe ni mshirika mwenyeji katika utekezaji wa mradi huu (Local
Project Partner), ambapo Jumuiya itatakiwa kutekeleza majukumu yote kama ilivyo katika hati ya makubaliano baina ya yetu na
Jumuiya ya ACRA. Miongoni mwa majukumu hayo ni kama
ifuatavyuo;
i.
JUHIMKO ndio atakayekuwa muhusiuka mkuu katika kupanga na
kutekeleza shughuli mbali mbalil zinazohusiana na kutoa taaluma na kukuza
uelewa juu ya masuala ya kihistoria na
urithi wa kiutamaduni uliopo Zanzibar .
ii. Pia JUHIMKO ndi
itakayoandaa mtaala utakaotumika katika shughuli za kutoa taaluma na elimu ya
kihistoria pamoja na umuhimu wa kuwa katika ramani ya urithi wa dunia kwa
walimu wa skuli mbali mbali za Zanzibar .
iii. Kuandaa na kufanya
kampeni, katika skuli mbali mbali zenye lengo la kutoa taaluma kwa ajili ya
kutoa muamko na kukuza uelewa juu ya masuala ya urithi wa kiutamaduni uliopo Zanzibar na kwengineko,
ambapo Jarida la UNESCO linalojuilikana kwa jina la (UNESCO Young Peoples World
Heritage Education Programme) litatumika pamoja na kutumia uzoefu kutoka kwa
JUHIMKO.
Ahsanteni
kwa kuniskiliza.
TAFSIRI YA UFUPISHO WA MANENO.
ACRA: Cooperazione
in africa e America Latina
AGSS: Associazione
Giovanni Secco Suardo
ZSTHS: Zanzibar Stone Town
Heritage Society.
JUHIMKO:
Jumuiya ya Hifadhi Mji Mkongwe.
SUZA: State University
of Zanziabar.
www.stonetownheritagesociety.wordpress.com face book:
www.facebook.com/zsths
No comments:
Post a Comment