Habari za Punde

Msaada wa kumsaidia Bi Mwanaid Vuai Saleh. aliyeunguwa kwa Maji ya Moto.

Kumradhini kwa kuweka picha hii ya Bi Mwanaid Vuai Saleh, kwa maadali ya habari haifai.
Aliyepata ajali hiyo ya  kuanguka wakati akiwa katika kazi zake za nyumbani na kuanguka katika sufuria la maji ya moto baada ya kuona kizunguzungu na kuangukia humo na kumuathiri kiasi hicho na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Jeshi Bububu akipata matibabu ya majaraha hayo.
Bi Mwanaid Vuai ni Mkaaza wa Shehia ya Chumbuni Wilaya ya Mjini Unguja 
Anaomba msaada wa Fedha ili kusafirishwa nje ya Nchi kupelekwa India kwav matibabu  zaidi 
Kwa kila Mwananchi atakayepata fursa ya kumsaidi Bi Mwanaid Vuai, ili kupata matibabu, anaombwa kuwasiliana na Mdau wa Blog hii, kwa Namba  0777424152.

 Bi Mwanaid Vuai Saleh akiwa ameathirika kiasi hicho kama anavyoonekanav pichani akiwa katika hospitali ya Jeshi Bububu Unguja akiendelea na Matibabu yake akisubiri misaada ya Wasamaria wema ili kupata kusafirishwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi ili kurudisha hali yake kiafya.
Kwa  sasa amepata baraka zote kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar kupata missada kama inavyosomeka hapo chini. 

9 comments:

 1. Subhana llah,Mwenyeezi mungu mpe afueni mja wako

  ReplyDelete
 2. smz ina mabilioni kujenga mnara wa upumbavu pale kisonge , vipi washindwe kumsaidia huyu mama?

  ReplyDelete
 3. Inasikitisha sana pia ni aibu kwa Serekali inayosema inawajali wananchi wake inakujali pale penye kampeni na upigaji kuraau kwenye propaganda zisizo na tija

  ReplyDelete
 4. SUNHANALWAH! ALLWAHU-AKBAR! MOLA AMPE SHIFAA. TUKO MBALI LAKINI NINA TIBA AMBAYO HUWASAIDIA WAGONJWA HOSPITAL NNAKOFANYA.NI MCHANGANYIKO WA MAZIWA FRESH I PKT+ 2FRESH BANANAS+I FULL RAW EGG+ ADROP OF BANANA FLAVOUR AND BLEND TOGETHER UNTILL THICK.THEN SIEVE AND SERVE AT LEAST TWICE A DAY. INAKAUSHA JERAHA NA KUEZESHA NYAMA MPYA KUMEA NA MPAKA NGOZI KURUDI KAMA ILIVYOKUA. NI HIGH PROTEIN DIET NA INATIBU HATA ALIEVUNJIKA MFUPA KUUNGA HARAKA. NA MAMBO MENGI MENGINE. INSHAALWAH MAABROUK------- FROM MOMBASA.

  ReplyDelete
 5. Pole sana dada yangu M.mungu mkubwa atakupa nafuu ya haraka na jaribu hiyo dawa uloambiwa ishallah utafanikiwa. Dada yangu mitihani tumeumbiwa sie wanaadamu ili M.mungu atupime subra yetu, muombe Alla atakusaidia.

  ReplyDelete
 6. mungu atakuafu dada

  ReplyDelete
 7. Subhana llah,Mwenyeezi mungu mpe afueni mja wako

  ReplyDelete
 8. Habari bwana Blogger?
  Naulizia maendeleo ya huyu mama anaendeleaje ? Jee michango ilitosha kwa ajili ya kumpeleka alikokusudia kwenda matibabu ?
  Na kama haikutosha tumepangaje kumsaidia au kuomba michango kumsaidia?

  Ni mimi CEO Kakytee MEdia

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.