Habari za Punde

balozi Seif Akabidhi Boti kwa Wananchi wa Kivunge

Mashua ya Riziki zina mola iliyonunuliwa na Serikali kulipwa fidia wavuvi wa Kijiji cha kivunge kufuatiwa mashua yao kuchomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali akimkabidhi Mashua iliopewa jina la Riziki Zina Mungu, kwa Ndg. Dhamiri Makame Juma, wa Kijiji cha Kivenge Wilaya ya Kaskazini Unguja, Mashua hiyoimeungwa katika Kijiji cha Nungwi Ungja.
  Mdhamini wa ujenzi wa Mshua ya Riziki zina Mungu Bwana Ali Makame Madaha { Cheupe } alitia saini hati ya kuuza mashua hiyo akishuhudiwa na Balozi Seif kwa ajili ya kupewa wavuvi wa Kivunge.
Balozi Seif ahesabu nusu ya fedha zilizoahidiwa kutolewa na serikali Milioni Nne { 4,000,000/- } kulipia fidia kutokana na mashua ya wananchi wa Kivunge kuchomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu. 
Picha na Hassan Issa wa – OMPR.


Na Othman Khamis Ame
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa shilingi Milioni Nne ikiwa ni nusu malipo ya gharama ya shilingi milioni Nane ilizoahidi kutoa kwa ununuzi wa Mashua  kwa ajili ya kufidia chombo cha Wavuvi wa Kijiji cha Kivunge   kilichochomwa moto mwezi Januri mwaka huu wa 2014 katika Kisiwa cha Tumbatu.

Ikasisitiza tena na kuonya kwamba hilo litakuwa ni tukio la mwisho kubebwa na Serikali la kulipa fidia kwa migogoro yoyote itakayosababishwa na wana jamii katika maeneo mbali mbali kutokana na hitilafu wanazoweza kuzikabili wana jamii wenyewe.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi fedha hizo kwa mdhamini wa ujenzi wa Mashua hiyo  Bwana  Ali Makame Madaha { Cheupe } hafla iliyofanyika pembezoni mwa bahari ya Nungwi ilipochongwa mashua hiyo Mkoa wa Kaskazini Ungua.

Balozi Seif alisema fedha hizo ni hatua ya kwanza na Serikali itajitahidi kukamilisha nusu iliyobakia katika kipindi kifupi kijacho itakayokwenda sambamba na wavuvi wanaohusika na suala hilo kupatiwa vifaa vyengine kama nyavu ili waendeleze uvuvi unaokubalika  Kiserikali.

Akipokea fedha hizo mdhamini wa ujenzi wa chombo hicho cha uvuvi ambae pia ni Katibu wa Kamati Tendaji ya hifadhi ya Mnemba na Chwaka Bwana Ali Makame Madaha { Cheupe } aliishukuru Serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kununua chomba hicho kwa wakati muwafaka.

Hata hivyo Bwana Madaha Cheupe alitahadharisha kwamba ongezeko la wavuvi katika baadhi ya sehemu hapa nchini ndio sababu kuu inayoleta migogoro ya uvuvi kwenye  maeneo mbali mbali ya bahari.


Aliiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuiongezea nguvu ya uwezeshaji Idara ya Uvuvi na mazao ya Baharini katika kubuni miradi mbadala itakayosaidia kukabiliana na msongamano huo wa wavuvi.

Akikabidhi rasmi chocho hicho kwa wavuvi wa Kijiji cha Kivunge na kushuhudia pia na Uongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wa Mkoa wa kaskazini Unguja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliendelea kuwaasa Wananchi kwamba Serikali kamwe haitakuwa tayari kubeba dhamana ya kulipa fidia ya mali au vyombo watakavyoharibiana kwenye migogoro wanayoweza kuiepuka.

Balozi Seif aliwahimiza Wananchi na hasa wavuvi katika maeneo mbali mbali nchini kuepuka ugomvi na pale yanapojitokeza mambo yenye kuleta hitilafu njia nzuri ni kukaa pamoja kwa pande husika katika mbinu za kuyapatia ufumbuzi muwafaka.

Tarehe 6 juni mwaka huu akizungumza na Wananchi wa Kivunge Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema tabia ya migogoro ya wavuvi ambayo inaonekana kuchochewa na baadhi ya wana siasa imekuwa ikiipa mzigo mkubwa Serikali kuu katika kugharamia fidia zisizo na msingi.

Balozi Seif alifahamisha kwamba  masuala ya maendeleo na kiuchumi kuingizwa mambo ya kisiasa kamwe hayatekelezeki na daima yataendelea kuwaharibia wananchi kimaisha.

Chombo hicho cha uvuvi walichokabidhiwa wavuvi wa kijiji cha kivunge kina uwezo wa kuchukuwa watu kwenda  katika shughuli zao za uvuvi kati ya ishirini na ishirini na tano kwa wakati mmoja.

Fundi wa chombo hicho Kilichopewa jina Riziki zina Mungu Rajab Haji Juma alitoa baraka na aliashiria kitendo cha kukishua  baharini chombo hicho tayari  kuanza safari ya kuelekea nyumbani katika kijiji cha kivunge.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.