Habari za Punde

Barabara za ndani za Mji Mkongwe kujengwa kwa kiwango cha lami

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uhifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar Ndg Issa Sarboko, akiwa na Ujumbe wa Wizara ya Ujenzi, ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa I. Iyombe, wakitembelea barabara za ndani ya Mji Mkongwe ili kuweza kukamilisha mradi huo wa ujenzi wa barabara hizo kupitia mradi wa Mbunge wa Jimbo la Mji Mkongwe. Mhe Ibrahim Sanya  
Moja ya Barabara za Mji Mkongwe katika eneo la majestiki cinema kuzunguka jengo hilo imo katika mradi huo kuzifanyia mategenezo kwa kiwango cha lami.
Mbunge wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar Mhe. Ibrahim Sanya akionesha moja ya barabara katika Jimbo lake akiwaonesha ujumbe kutoka Wizara ya Ujenzi Tanzania kufadhili ujenzi huo kwa kiwango cha lami kwa barabara za ndani za mji mkongwe, Barabara zitakazofaidika na mradi huo ni Masjesti, Vuga Malindi, Mkunazini na Mchangani.wakiwa katika eneo la majestiki akionesha barabara ya eneo hilo kwa ujumbe huo. 
           Ujumbe ukitembelea barabara za ndani za Mji Mkongwe Zanzibar kutadhimili ujenzi wake.

Barabara ya masjisti ilivyo sasa ikisubiri mradi wa barabara za ndani za mjimkongwe kutengenezwa na Wizara ua Ujenzi kupitia Mradi wa Mbunge wa jimbo hilo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uhidhafi ya Mji Mkongwe Zanzibar Ndg. Issa Sariboko, akionesha mipaka ya ujenzi wa barabara hiyo katika maeneo ya Mji Mkongwe ili kuweza kuhifadhi eneo la mjimkongwe likiwa katika hifadhi ya Kimataifa ya Utuzaji wa Miji Mikongwe Duniani.
Mbunge wa Mji Mkongwe Mhe Ibrahim Sanya akiwa na Ujumbe wake kutoka Wizara ya Ujenzi Tanzania wakikagua barabara hizo ambazo zitatengenezwa na Wizar ya Ujenzi Tanzania, kwa jitihada za Mhe Sanya  
Eneo la Barabara ya Vuga kuingia eneo la Ofisi za Bima na kutokea Shangani Branchi litafaidika na mradi huo.wa matengenezo ya barabara za ndani katika mji mkongwe Zanzibar.
Barabara za Ndani za Mji Mkongwe eneo la Vuga ikiwa katika mpango wa ujenzi wa kiwango cha Lami kupitia. Mradi huo.wa Mhe Mbunge wa Mji Mkongwe Sanya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Tanzania Eng. Mussa I Iyombe, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea barabara za mji mkongwe, ili kutathimini mradi huo ili kuaza kazi za ujenzi wake kupitia Wizara ya Ujenzi Tanzanai.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar Ndg, Issa Sariboko, akizungumza na waandishi baada ya ziara ya ujumbe huo kutembelea vianzio vya barabara za ndani za Mji Mkongwe, ili kuweza wakati wa ujenzi wake kufuata sheria za Uhifadhi wa Mji Mkongwe.   
Mbunge wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar Mhe. Ibrahim Sanya akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusiana na ujio wa Ujumbe huo kutoka Wizara ya Ujenzi Tanzania kukagua barabara hizo, Baada ya mazungumzo na Waziri husika wa Wizara hiyo.

2 comments:

  1. zikitiwa lami hao watalii watakuja kuangalia nini huko Zanzibar, na vile vigae vilotiwa vipi au vimeshinda kushuhulikiwa?

    ReplyDelete
  2. Barabara zinazotiwa lami si zile zilizotowa vigae barabara zinazotiwa lami ni zile za kuingia na kutoka katika mji mkongwe, kwa kutumia gari

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.