Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza msoma risala ya ufunguzi wa mchezo wa fainali ya mchezo wa Nage Kombe la Hamjad Jimbo la Chumbuni Zanzibar, iliozikutanisha timu za Masumbani na Kiungani, timu ya Kiungani imetoka na ushindi wa chupa 21--17.
Kamanda wa Vijana Jimbola Kwamtipura Ndg Ali Juma akizungumza na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Ndg. Othman Kibwana wakiwa katika viwanja vya masumbani wakisuhudia mchezo wa fainali ya mchezo wa Nage.
Mgeni wa Heshima Ndg Lulu Msham akiongozana na Kamanda wa Vijana Jimbo la Chumbuni Zanzibar Ndg. Hamjad, wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Kiungani ambayo imeobuka na ushindi wa Chupa 21-17 dhidi ya wapizani wao, Michuano hiyo imeshirikisha timu 12 katika jimbola Chumbini.
Mgeni wa Heshima Ndg Lulu Msham akiongozana na Kamanda wa Vijana Jimbo la Chumbuni Zanzibar Ndg. Hamjad, wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Masumbani, ambayo imeobuka na ushindi wa Chupa 21-17 dhidi ya wapizani wao, Michuano hiyo imeshirikisha timu 12 katika jimbola Chumbini.
Mgeni rasmin Ndg Lulu Msham akizingua mchezo huo wa fainali ya Kombe la Hamjad kwa mchezo wa Nage uliofanyika katika uwanja wa masumbani muembemakumbi,timu ya Kiungani imeshinda kwa Chupa 21-17
Mchezaji wa timu ya Masumbani akikwepa mpira katika mchezo huo.
Mchezaji wa timu ya Masumbanin askikwepa mpira katika mchezo huo wa fainali ya mchezo wa nage kati ya timu yao na timu ya kiungani.
Wananchi wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la Hamjad
Wachezaji wa tawi la Kiungani wakishangilia ushindi wao dhidi ya Masumbani kwa kuwafunga chupa 21--17.
Mdhamini wa michuano hiyo Kamada wa UVCCM Jimbo la Chumbuni Ndg Hamjad, akitowa nasaha zake kwa Vijana wa Jimbo lake wakati wa mchezo wa fainali la Kombe la Hamjad, lililofanyika katika viwanja vya masumbani na kuzikutanisha timu za Nage za tawi la Kiungani na Masumbani.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Lulu Msham akiwahutubia Vijana wa CCM wa Jimbo la Chumbuni baada ya kumalizika kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Hamjad, uliofanyika katika uwanja wa masumbani muembemakumbi Zanzibar, timu ya Kiungani imeshinda 21--17
Mgeni Rasmin wa Mchezo wa fainali ya Kombe la Hamjad, Ndg Lulu Msham, akimkabidhi zawadi yao mshindi wa Pili wa Michuano hiyo Nahodha wa timu ya Kiungani Ndg.Maryam Abdi shilingi laki mbili na kila mchezaji amepata doti ya kanga.katikati mdhamini wa Michuano hiyo Kamanda wa Jimbo la Chumbuni Ndg. Hamjad
Mgeni Rasmin wa Mchezo wa fainali ya Kombe la Hamjad, Ndg Lulu Msham, akimkabidhi zawadi yao mshindi wa Pili wa Michuano hiyo Nahodha wa timu ya Masumbani Ndg. Kazija Ame shilingi laki moja na kila mchezaji amepata doti ya kanga.
Mwanyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Ndg Othman Kibwaana akitowa nasaha zake kwa Vijana wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Hamjad.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifuatilia mchezo wa fainali kati ya Masumbani na Kiungani uliofanyika katika kiwanja cha masumbani muembemakumbi.
Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Hanjad Mchezo wa Nage Jimbo la Chumbuni Unguja wakimsikiliza mgeni rasmin akitowa nasaha zake kwa wanamichez wa jikmbo hilo baada ya kumalizika kwa Fainal ya Mchezo wa Nage Kombe la Hamjad, uliozikutanisha Timu za Tawi la Masumbani na Tawi la Kiungani, timu ya Kiungani imeshinda kwa chupa 21-17
Baada yakuripua Bomu katika Msikiti na Kuwa Mtu mmoja sasa Wanafurahia kwa Mchezo wa Nage..
ReplyDeleteInalilah wainailaihi Rajiun..
Inasikitisha kuona kwamba Wenzetu kule Upande wa Tanganyika wameamka na mambo ya maendeleo ya Miundo mbinu . Vijana wanajiajiri wenyewe na kuna vikundi vingi vya ushirika private NGOs ambazo zinawasaidia community zinazotaka kujikwa mua kiuchumi na kijamii..
Zanzibar tunaloliona ni Mchezo wa Nage, Kutoa Uniform za Mipira ya Maskani na upumbavu mwengine kama ule Wakukaa majukwaani na kutukana Viongozi na Uchochezi wa Ubaguzi.... Sasa tutegemee nini katika SMZ na mtindo huu wa Nage.
Mtu anecheza Nage akaka kati kati ya uwanja wa Mamluki na kupeta Maziwa ni mtu Muflisi aliekua hana jengine lakufanya isipokua kutumiliwa na Hao UVCCM ili yao yawaendee.
Anonymous 1. Umesema kweli ndugu yangu. Hata mimi bado najiuliza hivi kweli kwa mind-set kama hizi za hao wanaoitwa viongozi wa mitaa, majimbo, wilaya na hata serikali kuu kweli tutafika??
DeleteViongozi ni walezi wa jamii, inashangaza viongozi tena waislam waliotoka kwenye mifupa ya kiislaam toka enzi na enzi, leo wanawakusanya wanawake na kuwavua nguo eti (kuwachezesha nage) tena hadharani kabisa. Halafu maadili yakizidi kuporomoka sijui tumlaumu nani. Kwa kweli hasa Zanzibar bado hatujapata viongozi makini katika nyanja zozote zile. NI pumba tuu, ufuska na kudidimiza maadili mema ya kiislaam.
Inasikitisha. Walipaswa hao wanaoitwa viongozi kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili vijana (badala ya kukaa na kucheza/kutizama nage nakupoteza muda tu na hatimae kufanya yasiyo faa) wapate ajira.
Kwa style hii ya viongozi !!!???