Na Abdi Suleiman, Pemba
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Ali Iddi, amewataka wafanyabiashara katika soko la Wete kuendelea na
biashara zao, licha ya mfanyabiashara mmoja maarufu, Ahemd Abdalla (Mapete)
kudai anamiliki eneo hilo .
Alitoa kauli hiyo, baada ya kusikiliza
pande zinazovutaka katika mgogoro huo, ambazo kila upande unadi kumiliki eneo
lililpo soko hilo .
Pande zinazovutana ni serikali ya mkoa wa
kaskazini Pemba na mfanyabiashara huyo maarufu mjini Wete na kisiwani Pemba .
Alisema serikali ndio itakayotoa jibu juu
ya mgogoro wa eneo hilo
ambalo kwa sasa liko chini ya baraza la mji Wete.
Alimtaka mfanyabiashara huyo anaedai
kuuziwa eneo hilo na Katibu wa baraza la mji, ambaye kwa sasa ni marehemu kujua
kwambwa wote wana makosa kwani wameuza na kununua mali ya serikali.
“Eneo
hili ni mali ya serikali, limekabidhiwa baraza la mji Wete, sasa huyo mtu
aliyekuuzia yeye kafanya makosa na wewe umefanya kosa, kwani mumeiba mali ya
serikali,”alisema.
Alisema kwa sasa suala hilo linashughulikiwa
na serikali, hadi pale itakapotoa kauli nani mmiliki halali wa eneo hilo, hivyo
alimtaka mfanya biashara huyo kutokulitumia kwa kazi yoyote eneo hilo .
Kwa uapande wake, Katibu wa baraza la mji
Wete, Faki Hamad Faki, alisema eneo hilo ni mali ya
serikali tokea Mapinduzi ya 1964.
Alisema hakuna nyaraka zozote
zinazothibitisha kwamba Mapete ameuzia eneo hilo
na aliekuwa Katibu wa baraza hilo .
No comments:
Post a Comment