Na Bakar Mussa, Pemba
Uchunguzi wa Majina , Idadi wa Watu, majina
na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi Zanzibar, unaotarajiwa kufanywa na Tume ya
Uchaguzi Zanzibar, ni matakwa ya
Kikatiba ambayo yalianza kwa muda mrefu uliopita, pamoja na Tume hiyo kuchelewa
kufanya hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha,huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi
Pemba, wakati alipokuwa akizungumza na Wadau wa Uchaguzi wakiwemo Viongozi wa
Vyama vya Siasa , Taasisi za Serikali, na Wadau wengine juu ya matagemeo ya
Tume ya kufanya hivyo.
Mwenyekiti huyo , alisema kuwa ili kufanya
kazi hiyo , mashirikiano ya pamoja yanahitajika kwa kila mmoja ili kuweza
kufanyika kwa kazi hiyo muhimu kama Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza kifungu
cha 120 cha Katiba.
“ Kazi tunayoitarajia kufanya sisi Tume ya
Uchaguzi (ZEC), si matakwa yetu bali ni Katiba ya Zanzibar , ndio
inayotuelekeza kufanya hivyo pamoja na kwamba tumechelewa,”alieleza Mwenyekiti.
Nae,Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi
(ZEC),Salim Kassim Ali, alisema kuwa ili kuweza kuifanikisha kazi hiyo muhimu
kwa Taifa inategemea kupata maoni ya Wadau waliomo katika Majimbo ya Uchaguzi
kama ilivyohivi sasa katika Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba.
Alifahamisha kuwa ili kuweza kufanikisha
vyema kazi hii Tume ya Uchaguzi Zanzibar, imeandaa utaratibu maalumu wa
kukusanya Maoni hayo juu majimbo kwa taasisi na
Watu ambao hawatapata nafasi ya
kutowa maoni yao katika mikutano hiyo wanaweza kutowa maoni yao kwa maandishi.
Aidha , alisema kuwa Tume ya Uchaguzi
inatarajia kulieka Wazi Daftari la Kudumu
la Wapiga kura katika Majimbo yote ya Uchaguzi Zanzibar, kuanzia tarehe
21 hadi 26 /6 mwaka huu, ili kupata maboresho ya Daftari hilo na kueka sawa ili
kuondosha malalamiko yasiokuwa ya lazima.
Ayoub Bakar Hamad, Mjumbe wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC),itaendelea kuwashirikisha Wadau wake wa Uchaguzi kwa
kila jambo linalohusiana na Uchaguzi , kwa kufanya hivyo ni kupanuwa wigo wa Demokrasia nchini,
na hilo litakalofanyika ni matakwa ya kikatiba na kamwe sio matakwa ya Tume
hiyo.
Alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi itazingatia
na uzito uzito wa hoja za msingi na sio idadi ya watu watakao towa maoni yao ,
nan i vizuri maoni yakitolewa kwa maandishi ambayo ytasaidia Tume hiyo katika
kufanya uhakiki wake vizuri na kwa Uwazi.
“ Taasisi zitazopata fursa ya kutowa maoni
hayo ni vyema wakatowa yaliofananakwa pamoja ili kuondowa mgongano katika
Taasisi zao,” alieleza, Mjumbe huyo.
No comments:
Post a Comment