Habari za Punde

Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Kisiwani Pemba.

 
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi-Zanzibar (ZEC),Salim Kassim Ali, akitowa maelezo juu Mkutano wa Wadau wa Uchaguzi na Tume juu ya Ugawaji wa Majimbo Zanzibar.

 
Wanasiasa wa Vyama mbali mbali wakifuatilia kwa makini madhumuni ya Mkutano wa Tume ya Uchaguzi na Wadau huko katika Hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba.

 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) Jecha Salim Jecha, akifunguwa mkutano wa Wadau wa Uchaguzi huko katika Hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba.

 
Wakuu wa Mikoa miwili ya Pemba, Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa, na Dadi Faki Dadi, wakisikiliza kwa makini madhumuni ya Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Kisiwani Pemba.Mratibu wa Chama cha CHADEMA, Pemba, akitowa maelezo juu ya mashirikiano madogo baina ya Tume na Chama chake, huko katika Hoteli ya Hifadhi Kisiwani Pemba.
Picha na Bakar Mussa-Pemba.

1 comment:

  1. hivi visiwa vyote ukivikusanya ukubwa wake haufikii hata nusu ya Dar es salaam , sasa sielewi hivi kutaka kuongeza majimbo kuna umuhimu gani kama sio kuongeza gharama na mzigo kwa wananchi wenye kulipa kodi , ukiongeza majimbo maanake utaongeza ruzuku za uchaguzi kwa vyama , gharama za kuendesha chaguzi , mishahara na marupurupu atayolipwa huyo mwakilishi /mbunge watakaechaguliwa , kama watu hatuna akili za kuzaliwa basi tutumie angalao tulizopata skuli

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.