Habari za Punde

Waziri Aboud Afungua Ijitimai ya 20 ya Kimataifa kwa Niaba ya Rais Kikwete Fuoni Migombani Zanzibar.

Shekh Suleiman Rashid, akisoma Quran wakati swa ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa ya 20, inayofanyika katika viwanja vya  Ijitimai Fuoni Zanzibar na kuhudhuriwa na Waumini wengi kutoka Zanzibar na nje ya Zanzibar, Tanzania, Kenya, Uganda, Burudi,Malawi Zambia,wakishiriki Ijitimai hiyo iliofunguliwa leo na itakuwa ya siku tatu.
 Amir Kombo akitowa  tAfsiri ya Quran iliosomwa wakati wa Ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa ya 20 iliofanyika katika Viwanja vya Ijitimain Fuoni Migombani Zanzibar. 
Viongozi wa Dini na Wageni waalikwa katika Ijitimai ya Kimataifa ya 20, inayofanyika katika viwanja vya Ijitimai Fuoni Migombani Zanzibar, wakimsikiliza Waziri wa Nchin Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia  na kufungua Ijitimai hiyo


Mkalimali wa lugha kwa kutumia  alama za vitendo akitoka ishara hiyo kwa Waumini wasiosikia waliohudhuria katika Ijitimai hiyo  


Amir Wakati akitowa maelezo ya Makusudio ya Ijimai hii kwa Waumini waliohudhuria wakati wa ufunguzi wake.

Waumini wa Dini ya Kiislam wakifuatilia ufunguzi wa Ijitimai ya 20 ya Kimataifa inayofanyika katika viwanja vya Ijitimai Fuoni Migombani Zanzibar na kuhudhuriwa na Waumini kutoka nchi za Afrika Mashariki
Katibu wa Kamati ya Ijitima Zanzibar, Shekh Mwalim Hafidh, akitowa  maeklezo ya Ijitimai hiyo wakati wa Ufunguzi, uliofanyika katika viwanja vya Ijitimai Fuoni Migombani Zanzibar
Waumini wakimsikiliza Muft Mkuu wa Zanzibar akitowa nasaha zake, wakati wa ufunguzi a Ijitimai ya Kimataifa. 
Amiri Mkuu wa Ijitimai Zanzibar Shekh. Ali Khamis, akitowa risala ya maandalizi ya Ijitimai ya 20, wakati wa ufunguzi wa Ijitimai hiyo iliofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud, alifungua kwa niaba ya Rais Kikwete
Amiri Mkuu wa Ijitimai Zanzibar Shekh. Ali Khamis akimkabidhi Ramani ya jengo la Watoto Yatima wanaoishi katika Markas ya Ijitimai Fuoni Mhe. Mohammed Aboud, ili kuiwakilisha kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Jakaya Kikwete.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Kabi,akitowa nasaha zake wakati ya Ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa ya 20, iliofanyika katika viwanja vya Ijitimai Fuoni migombani Zanzibar jana
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud, akifungua Ijitima ya 20 ya Kimataifa Zanzibar, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, inayofanyika katika viwanja vya IjitimainFuoni Migombani Zanzibar
Waumini wa Kiislam wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Ijitimai ya 20 ya Kimataifa inayofanyika katika viwanja vya Ijimai Fuoni  migombni Zanzibar.
Amir Kombo akisoma dua baada ya hafla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika katika viwanja vya Fuoni Ijitimai Zanzibar.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua baada ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika kwa muda wa siku tatu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.