Habari za Punde

Ufunguzi wa Kongamano la Kupata Maoni ya Wadau kuhusu Rasimu ya Sera ya Petroli

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limejumuisha wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini
 Dar es Salaam. 
Wakuu wa mikoa ya Mbeya Abbas Kandoro (katikati) na Lindi Ludovick Mwananzila( kushoto) na Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Nishati Adam Zuberi (kulia) wakisikiliza  mada ya  rasimu ya sera ya Petroli iliyokuwa inatolewa leo katika kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu hiyo lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. 
Kamishna wa Nishati Eng. Hosea Mbise akiwasilisha  mada kuhusu rasimu ya sera ya Petroli kwa wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na  mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa  wakati wa kongamano la kupata maoni ya wadau lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. 

Kamishna wa Nishati Eng. Hosea Mbise (kushoto) akimpongeza  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro mara baada ya kufungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na  mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na  mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika jijini Dar es Salaam
Waandishi wa mkutano  (Rapporteur)  wakiandika  taarifa mbalimbali wakati wa  kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
(Picha na Anna Nkinda- Maelezo)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.