Habari za Punde

Mwanahabari ajitosa uchaguzi Chadema


Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar. (Picha zote na Martin Kabemba)

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza
kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyoJumamosiAgosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar.
Mbunge wa CHADEMA viti Maalum wa CHADEMA Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzaibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar.

Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
kundi la Zanzibar akitia saini kitabu chawageni mara baada ya kuwasili katika ofisi Kuu za chama hicho Zanzibar kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Na Martin Kabemba, Zanzibar

Mmoja wa wanahabari na mtangazaji mahiri wa wakati huu Salum Mwalim ameomba kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia nafasi za Zanzibar.

Uamuzi huo wa Mwalim ambae kwa sasa ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom tayari umeibua mjadala Zanzibar na kwamba unatarajiwa kubadili upepo wa uchaguzi wa Chadema Visiwani humo kutokana na ushawishi na mvuto alionao utakaomfanya kukubalika na kuaminika huku akifanya joto la uchaguzi kupanda.

Kwa sasa joto la uchaguzi ndani ya Chadema linaonekana kuwa juu zaidi Tanzania Bara.


Akichukua fomu ya kuomba kugombea kuingia kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi ndani ya Chadema, Mwalim amesema baada ya kushawishiwa na watu wa rika na wa aina mbalimbali kushauriana na makundi mbalimbali amejipima na kuona kuwa anatosha katika nafasi hiyo.

Mwalim amesema wakati wote wa maisha yake amekuwa akitembea na uzanzibari wake na kwamba alitambua kuwa siku moja atakuja kuwatumikia wazanzibar na hivyo kutoa mchango wake katika maendeleo ya visiwa hivyo ambako ndiko asili yakeilipo.

Mwalim amechukulia fomu hiyo mapema leo (Jumamosi Agosti 30) katika ofisi kuu za Chadema Zanzibar na kuirudisha majira ya mchana ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya uchukuaji wa fomu na urejeshaji kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho,

“Nimechukua fomu na sasa nairudisha, kwa kuwa wakati wa kampeni bado sitoweza kuzungumza wala kujinadi naomba niheshimu taratibu na miongozo ya uchaguzi ya chama lakini nataka kuwaambia kuwa Zanzibar na U-zanzibari wangu nijambo ninalojivunia kuliko kitu kingine chochote maishani mwangu.”Alisema Mwalim 
“Ni uamuzi mgumu sana kuwahi kufanya katika maisha yangu lakini nimeufanya kwa kuzingatia masilahi mapana ya chama ninachokiamini na kwa nchi yangu ya Zanzibar na watanzania kwaujumla.Ninamuomba Mwenyezi Mungu anisimamie anipe nguvu,afya,hekima,busara,unyenyekevu na uadilifu katika safari hii ya siasa ninayoianza.” Aliongeza Mwalim.

Akiongea kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa, amesema ana imani kubwa kuwa ataungwa mkono na kushinda nafasi hiyo kwa kuwa pande zote mbili za Visiwani naBara wanamfahamu vizuri sana na wanatambua mchango wake kwa Chadema na kwa nchikwa ujumla.  

Mwalim ambae ni msomi wa masuala ya uandishi wa habari na mwenye shahada ya uzamii katika usimamizi wa Biashara ni mmoja wa vijana waliotokea kujizolea umashuhuri mkubwa nchini kutoka na uwezo wake na uchapaji kazi wake akiwa mtu mwenye misimamo na kukubalika hasa na vijana nchini.

Kamati kuu ya Chadema ndicho chombo kikuu cha maamuzi ndani ya Chama hicho, naiwapo Mwalim atafanikiwa kushinda na kuingia kwenye chombo hicho anatabiriwakuwa atabadili upepo wa Chadema katika siasa za Zanzibar kutokana na Mwanahabari huyo kukubalika katika jamii na upya wake katika siasa unamfanyakuingia katika siasa pasi na kuwa na makundi hali itakayomwezesha kupewa ushirikianona kila mtu ndani na nje ya Zanzibar.
Akimkabidhi fomu hiyo Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar wa Baraza la Wazee La Chadema Bi Maryam Ahmed Omar amempongeza Mwalim kwa uamuzi wake huo na kumtakia kila la kheri katikauchaguzi huo.

Bi Omar amesema Chadema ya sasa imeimarika kwa kiwango cha juu na kwamba uamuzi wa Mwalim ambae ni kijana mzaliwa wa visiwani humo wa kuamua kugombea nafasi hiyo utasaidia kuongezanguvu ya kukiimarisha chama.

Tukio la uchukuaji wa Fomu wa Mwalim limehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Jumbe, mbunge wa wa viti maalum wa chama hicho Mwanamrisho Abama miongoni mwa viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.