Habari za Punde

Kilimani City Bingwa wa Kombe la Bima Zanzibar

Katibu Mstaaf wa ZFA  Mzee Zam akimkasbidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Bima Zanzibar Nahodha wa timu ya Kilimani City Mohammed Haji baada kuibuka bingwa wa michuano hiyo katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Mao, kati ya timu ya Black Sailors na Kilimani City, timu ya Kilimani City imeshinda 2--0.
Wachezaji wa timu ya Kilimani City wakishangilia Ubingwa wao baada ya kukabidhiwa Kombe hilo na Katubu Mstaaf wa ZFA Mzee Zam Ali, katika uwanja wa mao baada ya kuifunga timu yua Black Sailors 2---0.
Mshambuliaji wa timu ya Black Sailors akimpita beki wa timu ya Kilimani City wakati wa mchezo wa fainalio ya Kombe la Bima Zanzibar uuliofanyika uwanja wa Mao.
Mshambuliaji wa timu ya Black Sailors akizuiya mpira na huku beki wa timu ya Kilimani City akijiandaa kumzuiya.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimani City akizuiya mpira na kujiandaa kumpita mchezaji wa timu ya Black Sailors, wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa mao.
                         Beki wa timu ya Kiliomani City akiondoa mpira golini kwake.
                     Wachezaji wa timu ya Black Sailors na Kilimani City wakiwania mpira.

                 Kizazaaa golini kwa timu ya Black Sailors, wachezaji wakiwania mpira
Mshambuliaji wa timu ya Black Sailors akimpita beki wa timu ya Kilimani City katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Bima Zanzibar, mchezo huo umefanyika uwanja wa mao.
Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Zanzibar Ndg Issa Ahmada akitowa maelekezo kwa waamunu wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Bima Zanzibar kati ya Kilimani City nas Black Sailors uliofanyika uwanja wa Mao.
Kocha wa timu ya Kilimani City akitowa maelekezo kwa wacvhezaji wake wakati wa mapumzioko ya kipindi cha kwanza, Timu hizo zikiwa sare bila ya kufungana  
Kocha wa timu ya Black Sailors akitowa maelekezo kwa wacvhezaji wake wakati wa mapumzioko ya kipindi cha kwanza, Timu hizo zikiwa sare bila ya kufungana 



Viongozi wa timu ya Black Sailors wakiwa na mshangao baa pibda timui yao kukubali kipigo cha mabao mawili ya harakaharaka katika kipindi cha pili cha mchezo huo wa fainal ya kombe la bima Zanzibar.




2 comments:

  1. tunazishukuru mamlaka ya udhibiti wa biashara za bima TIRA Zanzibar kwa kutoa 500,000/- kwa washindi, Star investment (Z) ltd kwa 100,000/- kwa mfungaji bora na startimes kutoa king'amuzi kwa Bingwa wa mashindano hayo. Mungu awazidishie mooyo wa imani na mwakani wayaunge mkono mashindano haya yafane zaidi na zaidi.

    ReplyDelete
  2. its a first step but we would like to see more, as this firms they generate money also get tax concessions, and honestly the investment or prize money offered is nothing compared to how its done in dar, this is a first step and next step is to change the perception and more cooperative societies set up, we will be able to control demand and supply they will be paying alot to get our referrals, slowly and surely time will reach!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.