Habari za Punde

ZANZIBA YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA SIKU YA WAKUNGA SAMBAMBA NA KUZINDUA JUMUIA YA WAKUNGA ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akikata utepe kuzindua Katiba ya Jumuiya ya wakunga Zanzibar mara baada ya kuizindua jumuiya hiyo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidh Akipokea zawadi maalum kwa niaba ya  mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi kutoka kwa Katibu Mkuu wizara ya afya dk. Habiba Hasan Omar katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani ambayo hufanyika mei 5 Kila mwaka ,Kwa zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Mjini Unguja.

Baadhi ya wakunga wakila kiapo cha utii katika maadhimisho ya siku ya wakunga dunini ambayo hufanyika mei 5 Kila mwaka ,Kwa zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Mjini Unguja.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidh akizungumza kwa  niaba ya  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani ambayo hufanyika mei 5 Kila mwaka ,Kwa zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Mjini Unguja.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakunga Zanzibar Sanura abdalla Salim akitoa salamu za Jumuiya wakati wa  maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani ambayo hufanyika mei 5 Kila mwaka ,Kwa zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Mjini Unguja.

Biasha Mkamba Khamis akielezea matokeo ya uchunguzi wa lishe Kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18-25  wa shehia  mbalimbali za Unguja na Pemba    uliofanyika katika siku za kuelekea maadhimisho ya  siku ya wakunga Duniani ambayo hufanyika mei 5 Kila mwaka ,Kwa zanzibar maadhimisho hayo yamefanyika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Na Fauzia Mussa, Maelezo. 05-05-2024.

Mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi amewataka wakunga nchini kuwa na upendo, huruma na kufuata maadili ya taaluma zao ili kutoa huduma bora kwa mama wajawazito wakati wanapokwenda kujifungua.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh kwenye  Maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani huko  ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni amesema Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha afya ya uzazi ili kupunguza vifo vya mama na Watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.

Mama Maryam ambae pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Maisha bora foundation  ametoa wito wa kutokuachiwa na  kuonewa muhali  wanaonyanyasa wagonjwa na badala yake wachukuliwe hatua za kisheria.

Amesema wakunga wanamchango mkubwa katika kufanikisha malengo yaliopangwa na Serikali sambamba na kuiomba jamii kuwatumia wakunga hao ili kuepuka matatizo yanayoweza kuepukika.

Amefahamisha kuwa katika kuhakikisha huduma hizo zinazidi kuimarika Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteuwa Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga kwa lengo la kuweka usimamizi na kuleta mabadiliko katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa hasa mama na mtoto.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Habiba Hasan Omar amesema Wizara inaimarisha vituo vya Afya ya Msingi ili kumaliza tatzo la mama na mtoto na kusema kuwa Wizara ina mpango wa kuongeza watendaji katika maeneo yote ili kupunguza changamoto ya upungufu uliopo katika maeneo hayo.

Hivyo kuwataka watendaji wa kada hizo kuendelea kufanya kazi kwa umakini zaidi na huku Serikali ikiendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo hatua kwa hatua.

Sambamba na hayo amesema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwatumia wafanyakazi wa afya ngazi ya jamii (CHW) na kuwapa elimu ya lishe ili kuimarisha huduma za mama na mtoto pamoja na  kuwapatia mafunzo ya msingi ya dharura kwa mama wajawazito.

Akizungumza kwa niaba ya wanajumuiya ya wakunga Mkunga bi Sanura abdalla Salim amesema Lengo la kuanzishwa Jumuiya hiyo ni kuisaidia Serikali kuimarisha huduma za Afya hasa ya mama na mtoto.

Amefahamisha kuwa wamejipanga kuimarisha utoaji wa huduma bora za ukunga ili kuendeleza heshima ya wakunga na kutetea haki za wajawazito ikiwemo kupatiwa huduma zenye heshima za uzazi katika jamii na kwenye vituo vya afya Unguja na Pemba.

Aidha ameeleza kuwa wakunga wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa elimu ya utambuzi, upungufu wa vitendea kazi kama vile vifaa vya kisasa vya kusikiliza mtoto tumboni, Uhaba wa wakunga na wauguzi katika baadhi ya maeneo ya kutolea huduma za mama na mtoto.

Hivyo wameiomba Wizara ya Afya kuwaangalia watendaji hao kwa jicho la huruma kwani wanafanyakazi kubwa na ngumu ya kuhakikisha mama na mtoto wanabaki salama.

Maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani huadhimishwa Kila ifikapo mei 5  duniani kote ambapo kwa  Zanzibar maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya wakunga na Kauli mbiu ni "wakunga ni suluhisho muhimu ya mabadiliko ya Tabia Nchi".

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.