Habari za Punde

Ligi Kuu Zanzibar Malindi na KMKM imeshinda 2--1

Kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligu Kuu ya Grand Malt mwaka jana Timu ya KMKM, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa kwanza kuanza na timu ya Malindi uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya KMKM imeshinda 2--1 dhidi ya timu ya Malindi  
Kikosi cha timu ya Malindi kilicholazimishwa kukubali uteja kwa timu ya KMKM kwa kukubali kufungwa mabao 2--1.
Mshambuliaji wa timu ya Malindi Haji wa Haji akimpita beki wa timu ya KMKM Mwinyi Haji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt raundi ya kwanza mchezo uliofanyika uwanja wa amaan, timu ya KMKM imeshinda mchezo huo 2--1.Haji wa Haji mfungaji wa timu ya Malindi bao la kufutia machozi katika dakika ya 84 ya mchezo huo kipindi cha pili. 
Mshambuliaji wa timu ya Malindi Haji wa Haji akiruka kihuzi cha beki wa timu ya KMKM, katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika  uwanja wa amaan. timu ya KMKM imeshinda mchezo huo 2--1.
Golikipa wa timu ya KMKM Mudathir Khamis akidaka mpira wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya grand malt na timu ya Malindi ul;iofanyika uwanja wa Amaan jana.

Wachezaji wa timu ya KMKM na Malindi wakiwania mpira ukiwa juu kulia mchezaji wa timu ya Malindi Daud Suleiman na kushoto mchezaji wa KMKM Ibrahim Khamis.
Beki wa timu ya KMKM Khamis Ali kulia akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa timu ya Malindi Abdulsalam Othman, wakati wa mchezo huo wa ligi kuu ya grand malt iliofanyika uwanja wa amaan timu ya KMKM imeshinda 2--1. 




















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.