Habari za Punde

Ligi Kuu Zanzibar Miembeni yatoka sare na Chuoni 2-2

Na Mwajuma Juma

LIGI kuu ya Zanzibar iliendelea tena juzi huku sare zikitawala katika viwanja vyote viwili Unguja na Pemba.
 
Katika uwanja wa Amaan kulifanyika mchezo kati ya Miembeni na Chuoni ambao walitoka sare ya kufungana mabao 2-2 wakati sare kama hiyo ikitokea katika uwanja wa Gombani kati ya Timu ya Polisi na shaba.
 
Michezo hiyo ambayo ilichezwa majira ya saa 10:00 za jioni ambapo mchezo wa uwanja wa Amaan timu ya Chuoni ndio iliyotangulia kupata bao dakika ya kwanza kuanza kwa mchezo huo kupitia kwa Ibrahim Jeba na la pili likifungwa na Saleh Hamad dakika ya 84.
 
Kwa upande wa timu ya Miembeni mabao yake yalifungwa na Mkadam Ali katika dakika ya 56 na 89.
 
Huko Kisiwani pemba katika uwanja wa Gombani timu ya Polisi ndio iliyotangulia kupata mabao kupitia kwa wachezaji wake Mwita Mohammed dakika ya pili na Haule Innocent dakika ya 11, wakati Shaba wafungaji wake ni Mohammed Nyasa dakika ya 46 na Ali Suleiman Nuhu dakika 49.


Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo mmoja utakaochezwa katika uwanja wa Amaan kati ya timu ya Mafunzo na Malindi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.