Habari za Punde

Wananchi waaswa wanaponunua ardhi wahakikishe ziwe zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria

Na Mwajuma Juma
 
TABIA inayofanywa na baadhi ya watu kuuza ardhi kwa kutumia vielelezo visivyo sahihi imekuwa ikiipa wakati mgumu Serikali kwa kutumia muda mwingi  wa kutatua migogoro ya ardhi.
 
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati wakati akikabidhi kadi za usajili wa ardhi huko katika hoteli ya Bwawani mjini Unguja.
 
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ni lazima masheha na wananchi kuwa na tahadhari pamoja na kuwa makini na watu wa aina hiyo ili kuepusha migogoro.
“Siku  hizi kumeibuka baadhi ya watu wanaofanya vitendo hivyo kwa kutumia vielelezo visivyokuwa sahihi, vitendo ambavyo vinatupa wakati mgumu na kupoteza muda kwa ajili ya kutatua migogoro inayohusiana na ardhi”, alisema.

hivyo Waziri Shaaban aliwataka wananchi wanaponunua ardhi wahakikishe kuwa zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.


Alisema utoaji wa kadi za usajili wa ardhi umelenga kuhakikisha watu wote wanasajili nyumba na mashamba yao ili kupunguza migogoro hiyo na kuweka matumizi bora ya ardhi.

kwa upande wake Mrajis wa ardhi Zanzibar Bi  Mwanamkaa Abdulrahman, alisema zoezi hilo linaendelea katika maeneo mbalimbali ya zanzibar ambapo katika hatua ya awali, wamiliki 180 wa maeneo ya mji wamepewa kadi hizo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.