Na Masanja Mabula, Pemba
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha
Sheria Zanzibar, Jaji Mshibe Ali Bakar, ameitaka jamii kuacha tabia ya
kukimbilia mahakamani kupata haki kwa sababu kesi nyingi zinazofikishwa
mahakamani zinaweza kutatuliwa nje ya mahakama.
Amesema Tume hiyo imeamua
kutembelea maeneo yote ya Zanzibar kwa lengo la kutoa taaluma kwa jamii juu ya
sheria ili kusaidia kupungua mrundikano wa kesi mahakamani ambazo baadhi yao
hazina haja ya kufikishwa huko.
Akizungumza katika kikao
kilichowashirikisha wafanyakazi kutoka taasisi za serikali na ninafisi mkoa wa kaskazini
Pemba, alisema hakuna budi mwananchi anayetaka kupeleka shauri lake mahakamani
kujitambua kabla hajaliwasilisha.
“Baadhi ya kesi zinazofikishwa
mahakamani hazina mashiko, jambao ambalo linapelekea kesi kufutwa na baadae
wananchi kulalamika,” alisema.
Aliitaka jamii kubadilisha
kurejesha tabia inayopotea ya uaminifu hasa kwa wazee kutokana na kuongezeka
vitendo viovu vinavyofanywa na kundi hilo.
Akizungumzia uhusiano kati ya wakili
na mteja, Mwanasheria Khamis Mwita Haji, alisema lazima wakili aweze atunze siri
za mteja wake na anapaswa kumweleza mwenendo mzima wa kesi yake.
Akichangia katika kikao hicho,
Sheha wa shehia ya Mtemani Wete, Juma Mrisho Magogo, alisema bado baadhi ya
wazazi wanawaonea aibu watoto wao na kwamba wanashindwa kuwambia ukweli kuhusu
nyenendo zao.

No comments:
Post a Comment