Habari za Punde

Matukio katika Picha Vivutio vya Watalii Wanaofika Pemba.

 PAMOJA na makumbusho haya ya msikiti wa wahindi jamii ya mabohora, uliopo kijiji cha Jambangome wilaya ya Mkoani Pemba, kusemekana kama ndio eneo la mwanzo kuhamiwa kisiwani Pemba tokea karne ya 18 hadi ya 20, bado serikali kupitia Idara yake ya makumbusho hawajaona umuhimu wa kuyahiafadhi na kusababisa kuzongwa na pori na kupoteza fedha za kigeni
 
MKUU wa kamisheni ya utalii Pemba mwalimu Suleima Amour, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo lenye makumbusho ya waanzilishi wa kisiwa cha Pemba, wahindi jamii ya mabohora kwenye karne ya 18 hadi 20, kijiji cha Jambangome wilaya ya Mkoani Pemba, ambapo kamisheni ya utalii inaendelea na kampeni yake ya utalii kwa wote 

ENEO la Tandauwa wilaya ya Chakechake Pemba, ambapo panasemekana palikuwa na kisima cha utafiti wa mafuta kwenye miaka ya 1961, kazi iliofanywa na kampuni ya BP Schell, ambapo kwa sasa limebakia bila ya kuhifadhiwa 

GATI iliko kijiji cha bahari ya Tundauwa wilaya ya Chakechake Pemba, ambayo kwenye miaka ya 1960 hadi mwaka 1962 ilikuwa ikitumiwa na kampuni ya BP Schell kwa ajili ya kushushia vifaa na magari yao wakati walipokuwa wakiendesha utafiti wa mafuta kisiwani humo, ambapo kwa sasa gati hiyo inayoweza kuingizwa kwenye makumbusho ya taifa imetelekezwa. 
 KATIKATI Mkuu wa Kamisheni ya utalii Pemba mwalimu Suleiman Amour akiwa na mzee Mohamed Bakari Juma (71) ambae alikuwa akiutembeza ujumbe wa waandishi wa habari na watendaji wa kamisheni ya utalii, ili kutoa historia halisi ya kujengwa kwa gati hiyo kwenye miaka 1960 ili kampuni ya BP Schell kupitishia vifaa wakati ikifanya utafiti wa uchimbaji mafuta kijiji cha Tundauwa Pemba.
 KATIBU wa ‘’Wawi spice farm’ Ali Mohamed Ibrahim akizungumza na waandishi wa habari, juu ya malengo ya kuanzisha kituo cha utalii wa ndani, wakati waandishi hao walioambatana na watendaji wa kamisheni ya Utalii, walipofika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya kutangaaza utalii kwa wote. 
MWENYEKITI ushirika wa ufugaji samaki ‘Sir Fish Firm’ uliopo Pujini kibaridi aliembele Ahmed Salim Issa, akiuongoza ujumbe wa waandishi wa habari na watendaji wa kamisheni ya utalii Pemba, ili kuangalia ufugaji wa samaki, ikiwa ni ziara maalumu ya kuimarisha sera ya utalii kwa wote.(Picha na Haji Nassor Pemba)

1 comment:

  1. Habari nzuri ila jina la kampuni nadhani ni Shell na sio Schell

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.