Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni ametowa
changamoto kwa Wanasiasa kutatua matatizo ya Wananchi kwa vitendo badala ya
kutumia matatizo hayo na kero zao kwa kujinufaisha wao.
Amesema hayo wakati wa ziara yake kutembelea mradi mkubwa wa
maji safi na salama kwa Wananchi wa jimbo lake, baada ya kukamilika kwa Mradi
huo awamu ya kwanza ya uchimbaji wa kisima huko maeneo ya kaburi kikombe na
kutandaza mabpmba ya maji.
Mhe Masauni amesema mafanikio ya Mradi huo na miradi mengine
katika jimbo lake yametokana na nguvu za Wananchi kwa kutaka maendeleo katika
jimbo lao la kikwajuni yanayotokana na misaada na mashirikiano makubwa kati ya
wadau wa maendeleo wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Amesema mradi huo mkubwa wa maji safi na salama uko katika hatua
ya mwisho kwa kuweka miundombuni ya kusambaza maji, ya utandazaji wa mabomba ya
maji kwa sasa tayari utandazaji wa mabomba hayo yameshafika katika hatua kubwa
kwa kutandika eneo kubwa na kufikia katika hutua ya kuunganisha na tangi
lililoko mnara wa mbao kilimani.
Ufungaji wa Tangi jipya unatarajiwa kukamilika si muda mrefu na
ili kuhifadhia maji hayo na kusambaza kwa wananchi wa jimbo la Kikwajuni na
maeneo jirani. amesema tangi hilo lina uwezo wa kuhifadhi lita nyingi za maji
na kuondoa tatizo la maji katika jimbo lake.
Pia amewataka Wananchi kuunga mkono Katiba Mpya iliopendekezwa na
Bunge Maalum la Katiba lililomaliza kazi yake hivi karibuni na kukabidhi kwa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete na Rais wa Serekali
ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Dodoma.

No comments:
Post a Comment