Habari za Punde

Uboreshaji wa daftari la wapiga kura kuanza Novemba


IMG_8833
Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
…………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo,Maelezo
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema kwamba  zoezi la majaribio ya  Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linatarajia kuanza rasmi katikati mwa mwezi  Novemba mwaka huu.

Aidha  NEC imefafanu kwamba zoezi hilo, litafanyika kwa kutumia mfumo mpya wa ‘Biometric Voter Registration’(BVR) katika majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Kilombero, Halimashauri ya Mji wa Kilombero na Mlele, Halimashauri ya Mlele, ambapo vituo vya uandikishaji vimewekwa katika kata zilizomo katika majimbo husika.

Hayo yalisemwa  na Makamu Mwenyekiti wa NEC  pia  na Jaji  Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud  Hamid,wakati  akisoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam.

“Tume tayari imekwishapokea baadhi ya vifaa muhimu vya uandikishaji zikiwemo fomu za unadikishaji, hivyo kinachosubiriwa ni kupokea BVR kits 250 zinazotarajiwa kupokelewa wakati wowote kuanzia leo. Zoezi la Uandikishaji litakapoanza, vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni, vyama vya siasa vinaruhusiwa  kuweka mawakala wao katika kituo ili kushuhudia jinsi uandikishaji utakavyokuwa unafanyika,” alisema  Hamid.

 Makamu Mwenyekiti huyo alisema baada ya zoezi hilo kukamilika zoezi hilo litaanza katika maeneo mengine.

“ Tunatarajia Uboreshaji  wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa yote nchini isipokuwa mkoa wa Dares Salaam na Zanzibar.Uandikishaji katika mikao ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika baada ya uandikishaji katika mikoa yote utakapokamilika.Muda wa 
uandikishaji  utakuwa ni siku saba katika kila kituo,” alisema.

Aliongeza kwamba uandikishaji katika mikoa yote umepangwa kufanyika kuanzia mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu hadi katikati ya   Februari mwaka huu, wakati katika mikoa ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

 Alisema uandikishaji katika mikoa yote utafanyika katika awamu nne kwenye kila halimashauri ili kutoa fursa ya kuhamisha vifaa vya uandikishaji   kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.

“Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utahusisha  wapiga kura wote wapya na wa zamani. Wapiga kura wa zamani yaani wale ambao walikuwa wamejiandikisha katika Daftari la Zamani, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha vilivyoko karibu na maeneo wanayoishi ili kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole, picha na saini zao kuiongizwa katika mfumo Biometric Voter Registration na hatimaye watapewa vitambulisho vipya.” Alisisitiza.

Alisema wapiga kura ambao watakuwa na kadi zao za kupiga kura za zamani watatakiwa kwenda na kadi zao katika kituo cha kujiandikisha ili kurahisisha zoezi la kuhamisha taarifa zao za awali katika mfumo mpya wa BVR.

 Aidha alifafanua kwamba  kwa wapiga kura waliopoteza kadi au wale ambao kadi zao zimeharibika watatakiwa kwenta kituoni ili kujiandikisha na kupewa kadi mpya.

 Hamid alisema kwa wapiga kura wenye vitambulisho vya taifa Dares Salaam na Zanzibar watakuja na kadi zao ambazo ni taarifa zao zitasomwa na vifaa maalum ili kupunguza muda utakaotumika katika zoezi hilo, pia watapewa kadi mpya ya mpiga kura.

 Alisema kwa wapiga kura wanaoishi na ulemavu na wale ambao hawajui kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda kituoni na mtu mmoja katika familia wanayemuamini ili kusaidia katika uandikishaji.

“Uboreshaji huu unahusisha pia kuandikisha wapiga kura wote waliotimiza umri wa miaka 18 au zaidi na wale ambao ifikapo siku ya upigaji  kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 watakuwa wametimiza umri wa miaka 18. Pia wale wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuwahi kujiandikisha katika Daftari la  Kudumu  la Wapiga Kura katika mazoezi yote uandikishaji yaliyopita,” alisisitiza.

Hivyo jumla ya watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi wapatao milioni 23.09 wanatarajiwa kujiandikisha.

Hamid aliongeza kwamba mpiga kura atakayejiandikisha katika daftari hilo la sasa pekee na kupewa kadi ndiye atakayeruhusiwa kupiga kura.

“Wakati wa uandikishaji, kipaumbele kitatolewa  kwa watu wanaoishi na ulemavu, wazee, wagonjwa wakinamama wajawazito na wenye watoto wachanga. Hivyo hawatalazimika kusimama kwenye mstari.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka  NEC, Julias Malaba alisema tayari kiasi cha fedha cha Sh. bilioni 15 zimeshatolewa kwa ajili ya zoezi hilo.Huku Makamu Mwenyekiti wa NEC  akisema bajeti halisi litafafanuliwa baadae.

Kwa upande wake, Sisti  Cariah ambaye ni Mkuu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Naibu Katibu NEC, alisema daftari hilo litakamilika  Aprili 14,mwaka huu na litawekwa  wazi   kwa muda wa siku tano katika maeneo husika  ili kumwezesha kila mtu aliyejiandikisha  aende  kukagua na kujiridhisha kwa taarifa zake zimeandikwa  kwa usahihi.

 Tume hiyo inatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza kwa wingi katika vituo vyote vya uandikishaji kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari hilo.

Akizungumzia  kuhusu mfumo wa BVR alisema unasaidia kupunguza ujiandikisha mara mbili na kuwa na taarifa sahih

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.