Habari za Punde

Rais Kikwete azungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili akitokea Marekani kwa matibabu


Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waandishi wa habari uwanja wa ndege leo Jumamosi Novemba 29, 2014 mara tu baada ya kutua toka Marekani alipokuwa amekwenda kwa ajili ya upasuaji wa saratani ya tezi dume. (picha kwa hisani ya Michuzi)
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Wanahabari na kuwataarifu kwamba alichofanyia ni upasuaji  wa saratani ya tezi dume  na hili alilijua mapema kabla ya kuja nchini Marekani na lilikua si jambo rahisi kulielezea lakini nilikua sina budi kumweleza mke wangu wananagu wakiwemo ndugu zangu na baraza la Mawaziri walikua wanalifahamu hilo. Nilitaka kuwaambia wananchi pale nilipoongea na wazee Dodoma lakini nilishauriwa nisifanye hivyo badala yake tutangaze nakwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya.

Rais Jakaya Kikwete aliwashukuru Waandishi wa habari na watu wote waliomjulia hali kwa kupiga simu au kutuma ujumbe wa SMS wakati akiwa hospitali ya Johns hopkins iliyopo Baltimore, Maryland nchini Marekani. Pia Rais aliwaomba Watanzania waanzishe tabia ya kujiangalia afya zao kwani kwa kufanya hivyo ndio kulimsaidia yeye kugundua kwamba ana saratani ya tezi dume na kupona kwake ni kufanyiwa upasuaji.Rais amesisitiza hasa kwa wanaume unapofikia umri wa miaka 40 ni vizuri kujenga tabia ya kuangalia afya yako.

Rais Jakaya Kikwete alimalizia kwa kuawaambia waandishi habari kwamba leo hatalizungumzia yaliyopo Dodoma kwa sababu hayafahamu kwa kina lakini akaahidi mara atakapopata taarifa kamili atayafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.