Habari za Punde

Sherehe za Kuipongeza Timu za Michezo za KMKM viwanja vya Maisara

Mbio za kilomita 10 zikiaza katika eneo la Kibweni Ikulu lililowashirikisha wakimbiaji zaidi ya 330 wa Kimataifa wa Zanzibar na Wanamichezo wa vikundi vya mazoezi vya Kitambi noma wakiaza mbio hizo kuelekea katika viwanja vya maisara KMKM.
Wakimbiaji wa mbio za kilimita 10 wakiaza mbio hizo katika maeneo ya Kibweni Ikulu barabara ya bububu kuelekea viwanja vya maisara.
     Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mchezo wa mbio za kilimita 10 zilivyoaza kwa ushindani mkubwa.
Wakimbiaji kutoka Ndijani wanawakev wakishiriki mbio hizo za kilomita 10 wakionesha uvundi wao.
Wakimbiaji kutoka vikosi vya Ulinzi na Usalama wakishiriki mbio hizo wakioneshana ufundi.wakipita katika maeneo ya maruhubi wakiwa katika nafasi ya tatu na nne katika michuano hiyo ikielekea katika viwanja vya maisara.
Mshindi wa kwanza wa mbio hizo za kilimita 10 Filipo Jacob kutoka Mafunzo Zanzibar akiongoza mbio hizo akifuatiwa na mkimbiaji kutoka JWTZ Elia John, wakipita katika maeneo ya muembemakumbi kuelekea maisara kumalizia mbio hizo.
Mshindi wa mbio za kilimita 10 kutoka Kikosi cha Mafunzi Filipo Jacob, akimaliza mbio hizo kwa kuwa mshindi wa kwanza wa mbiuo hizo za kusherehekea Ubingwa wa Timu za Vikosi vya KMKM Zanzibar kwa kuchukua ushindi kwa miaka miwili mfululizo  
Mkimbiaji kutoka JWTZ Elia John, akisaidiwa kumaliza mbuio hizo baada ya kubana na misuli akiwa karibu kumaliza mbiop hizo katika viwanja vya maisara alikuwa akichuana na mshindi wa mbio hizo Filipo Jacob. 
Mkimbiaji wa Kike kutoka KMKM Aldina Edward akimaliza mbio hizo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwa wanawake walioshiriki mbio hizo.
Katika mbio hizo pia zimawashirikisha Wanamichezo wwenye ulemavu kama anavyooneka mwanamchezo Hadaa Khatib akimaliza mbio hizo katika viwanja vya maisara.
Mkimbiaji kutioka Japan Seiki Shinizy  akishiriki mbio hizo na kutchukua nafasi ya 45katika mbio hizo 
         Viongozi wa meza kuu wakifuatilia sherehe hizo katika viwanja vya KMKM Maisara
Maofisa Wastaaf wa KMKM wakivuta kamba na Maofisa wa KMKM katika sherehe hizo wakiongozwa na Kocha wao Mzee Haidar wakiongoza jinsi ya kufuta kamba na kushinda mara mbili na kujinyakulia fedha zilizotolewa na Mfanyabiashara Muhamadi Pande kwa mshindi wa mchezo huo na kujinyakulia shilingi laki tano zilizotolewa kwa mshindi wa mchezo huo.
Maofisa wa KMKM wakishindana kufuta kamba na Maofisa wastaaf wa KMKM hatimai kushindwa na Maofisa Wastaaf mara mbili ya mchezo huo. 
Maofisa waastaf wa KMKM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwashinda Maofisa wa KMKM katika mchezo wa kuvuta kamba na kujinyakulia shilingi laki tano zilizotolewa na Mfanyabiashara maaruf Zanzibar Muhamadi Pande kwa mshindi wa mchezo huo.

Mkim,biaji kutoka Kikundi cha mazorzi cha ZAFISA akimaliza mbio hizo katika viwanja vya maisara akishindikizwa na msimamizi wa mbio hizo 
Mkuu wa Kikosi Cha KMKM Komodoo Hassan Mussa, akizungumza katika uzinduzi wa kusherehekea Ubingwea na Timu za KMKM kwa miaka miwili iliochukuwa katika michezo. uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya KMKM maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanamichezo wa KMKM kwa kuwa mabingwa wa mchezo wa Mpira wa miguu za Ligi Kuu Grand Malt Zanzibar  kwa miaka 2012/2013 na 2013/2014. sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya mpira maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za kilimita 10 kwa wanawake kutoka KMKM Aldina Edward.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi yake mshindi wa kweanza wa mbio za kilimita 10 Wanaume Filipo Jacob
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi mshindi wa Pili wa mbio hizo kwa Watu wenyev Ulemavu Amina Daud.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Ofisa Mstaaf wa KMKM Ndg Fetei kwa ushindi wa kufuta kamba walikabidhiwa shilingi laki tatu zilizotolewa na Mfanya Biashara wa Zanzibar Ndg Muhamad Pande. kwa kuvutiwa na Maofisa hao wastaaf kwa kuwa na stamia ya kuhimili mikiki ya Vijana Maofisa wa KMKm katika mchezo huo.



                       Maofisa Wastaaf wa KMKM wakifuatilia michuano hiyo ya sherehe
                                Mambo ya mbwa kachoka hayoooooooooo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.