Na Augusta Njoji, Dodoma
Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu
kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kugonga lori kwa nyuma wakati ikitaka kuzpita gari zilizokuwa mbele yake.
Ajali hiyo ilitokea juzi majira
ya saa 12:30 jioni katika eneo la njia panda ya NARCO barabara kuu ya
Morogoro-Dodoma wilayani Kongwa.
Kamanda wa Polisi Mkoani
hapa,David Misime, alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T
213 DAR Toyota Mark X ambalo lilikuwa likiendeshwa na Hassan
Hussein (35), mkazi wa Dodoma likiwa na abiria wanne wakitokea Morogoro
wakielekea Dodoma.
Alisema gari hilo liligonga kwa
nyuma gari lenye namba za usajili T 963
BRC Leyland Daf lililokuwa na tela lenye namba T708 ASP likiendeshwa na Tumaini
Josia (23) mkazi wa Mbagala rangi tatu mkoani
Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu wawili pamoja na majeruhi watatu.
Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa
ni John Mmasi maarufu kwa jina la Matei (32),mmiliki
wa Matei Lounge ambaye alifariki njiani alipokuwa akikimbizwa hospitali ya rufaa
Dodoma na Joshua Oguda(32) wakili wa
kujitegemea aliyefariki akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa Dodoma.
Kwa upande wa majeruhi ni Bossi Ngasa (28),
Juma Zuberi (23), Hassan Hussein(35) aliyekuwa dereva wa gari dogo ambao wote wamelazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Dodoma wakiendelea na matibabu.
Misime alisema uchunguzi wa awali unaonesha
chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa
dereva wa gari dogo kutaka kuzpita gari zilizokuwa mbele bila kuchukua taadhari.
No comments:
Post a Comment