Na Tatu Makame
Wizara ya Kilimo na Maliasili
Zanzibar, imetumia jumla ya shilingi 25 milioni kununulia mashine ya kuchujia
mafuta ya alizeti, itakayowanufaisha wananchi wa maeneo mbali mbali ya kisiwa
cha Unguja.
Mashne hiyo ina uwezo wa
kusafisha mafuta dumu 100 za ujazo wa lita 20 kwa siku, mafuta ambayo hayana
aina yoyote ya kemikali.
Akizindua mashine hiyo katika
kijiji cha Bambi wilaya ya kati Unguja, Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar,Dk.
Sira Ubwa Mamboya,alisema kuwepo kwa mashine hiyo kutasaidia kupunguza tatizo
la ajira kwa vijana.
Aidha alisema,kuna vijana wengi
wanaosubiri ajira kutoka serikalini,hivyo mashne hiyo itasaidia kupunguza dhana
hiyo kwani vijana wataweza kujiajiri.
“Kuna vijana wengi wanaosubiri
ajira kutoka serikalini, hivyo kuwepo kwa mashine hiyo kutasaidia kupungua
tatizo la ajira kwa vijana,” alisema.
Alisema huu ni wakati mzuri wa
kubadilisha maisha ingawa Zanzibar ni nchi ndogo lakini endapo wananchi
watabadilika kuna uwezekano mkubwa wa kupata maendeleo.
Nae Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti kutoka
wizara hiyo, Mariam Juma Abdalla, alisema,wizara imechukua juhudi za kuwawezesha wakulima ili kuondokana na
umaskini.
Aidha alisema mabwana na mabibi
shamba 80 Unguja na Pemba wamepewa elimu ya kuwafundisha wakulima jinsi ya
kutumia mashine hizo.
Alisema wizara imo kwenye
mchakato kwa kutafuta mashine nyengine ili na wakulima wa kisiwa cha Pemba na
wao wafaidike,
Nao wakulima wa zao hilo, walisema
watahakikisha mashine waliyopewa wanaitumia ipasavyo ili kuendeleza kilimo cha
alizeti.
Usssi Yahya akizungumza kwa
niaba ya wakulima wenzake waliiomba serikali kuwapatia maeneo yanayoweza kuzalisha
alizeti ili kuinua uchumi wa nchi kwani mafuta ya elizeti yana soko kubwa.
No comments:
Post a Comment