Na Fatuma Kitima,DAR ES SALAAM
Kampuni ya Global Education
Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),Wizara ya Elimu
na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade)
wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa
kufanyika Disemba 10 hadi 14 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Global link Education,Abdulmalik Mollel,
alisema lengo la maonyesho hayo ni
kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa
wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.
Alisema ushiriki wa asasi
mbalimbali kwa kushirikiana na
sekta binafsi utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa
matokeo makubwa sasa.
Aidha alisema maonyesho hayo
yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani
katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Maonesho hayo yanatarajiwa
kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka
ndani na nje ya nch.
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘kuweka
jitihada za pamoja katika kuboresha mfumo wa elimu Tanzania ni njia thabiti ya
kuleta maendeleo endelevu katika taifa.’
No comments:
Post a Comment