Na Ameir Khalid
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.
Abdilahi Jihad Hassan, amesema shughuli za uvuvi zinapaswa kusimamiwa vyema,
ili vizazi vijavyo viweze kurithi rasilimali nzuri zitakazowasaidia katika
maisha yao ya baadaye.
Alitoa kauli hiyo katika ukumbi
ya hoteli ya Grand Palace Malindi, alipokuwa akizindua mpango mkakati wa
utawala na usimamizi wa shughuli za uvuvi Zanzibar, ukiwa na lengo la kuwa na
uvuvi endelevu.
Alisema shughuli za uvuvi zinapaswa
kusimamiwa vyema ikiwa ni mpango ambao utasaidia kuwa na lengo na nia ya matumizi mazuri na endelevu ya bahari ili
wavuvi na wananchi wa Zanzibar waweze kunufaika na rasilimali ya bahari iliyopo.
Alisema katika kuhakikisha
jambo hilo linafanikiwa ni vyema kuimarishwa mfumo wa utawala na usimamizi wa
kuwawezesha wavuvi wa kienyeji kuvua samaki katika bahari kuu.
Mapema Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Dk. Kassim Gharib Juma, alisema sekta ya uvuvi Zanzibar inachangia kwa
asilimia 7.1 katika uchumi wa Zanzibar, huku ikibainika kuwa asilimia kubwa
ya wavuvi wa Zanzibar wanatumia uvuvi wa
kienyeji.
Alisema mipango inayofanywa ni kuhakikisha
kunapatikana mafanikio makubwa ya uvuvi ifikapo mwaka 2020 malengo yote
yaliokusudiwa tayari yawe yametekelezwa
No comments:
Post a Comment