THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia
jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK),
Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa
Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu
Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu,
Dar Es Salaam.
Taarifa
hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston
Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako
anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa,
Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa
Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro
kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine
ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa
wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka
Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa
Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu
wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
6 Desemba,2014
Hii ni katika kuboresha utendaji!
ReplyDelete