Habari za Punde

Ujumbe wa wadi za Makunduchi safarini Sweden

Ujumbe wa wadi za Makunduchi waondoka leo kuelekea Kiruna Sweden. Ujumbe huo unaoongozwa na afisa tawala wa wilaya ya Kusini, ndugu Abdallah Ali Kombo, mwenye suti, utakuwa nchini Sweden kwa wiki moja kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya manispaa ya Kiruna na wadi za Makunduchi.
 
Wakiwa Kiruna watatembelea maeneo ya utalii na kufanya mazungumzo juu ya kuimarisha kituo cha kompyuta kilichopo Makunduchi. Aidha ujumbe huo utaendeleza mazungumzo ya kuimarisha elimu ya ujasiriamali yenye lengo la kuwatayarisha vijana kujiajiri wenyewe.

1 comment:

  1. iyo inafaa sana kwa maendeleo yetu lahe. kama kuna watu wanakona choyo na wadate vyo heya kae tuchavata maendeleo sana tukawa vamoja

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.