Mabati 250 yaliyotolewa msaada na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF
kwa ajili ya uezekaji wa madarasa saba, Stoo na Afisi ya Mwalimu Mkuu kwa Skuli
ya Sekondari ya Kangagani, jimbo la Ole Pemba.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari
Kangagani Omar Kombo Hamad (kushoto) akisoma maelezo ya ujenzi wa Skuli yao kwa
wajumbe wa kamati ya ujenzi na maafisa wa ZSSF katika hafla fupi ya kupokea
msaada wa mabati 250 yaliyotolewa na ZSSF na kugharimu TSh. 3,550,000/=.
Meneja wa ZSSF tawi la Pemba Bw. Rashid
Mohammed Abdullah (Kulia) akimkabidhi mabati 250 Kaimu Mwalimu Mkuu wa Skuli ya
Sekondari ya Kangagani kwa ajili ya kuezeka madarasa mapya ya kusomea na Afisi
ya Mwalimu Mkuu. Huu ni msaada wa pili wa ZSSF kwa skuli hiyo ambapo awali
iliwahi kukabidhiwa matofali zaidi ya 1000 kwa ujenzi.
No comments:
Post a Comment