Habari za Punde

Kinana akutana na ujumbe wa kamati kuu ya chama cha SPLM

utana




Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzana na Kamati Kuu ya Chama Cha SPLM ambapo alipeleka ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,kikao hicho kilikuwa chini ya Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir, Ikulu mjini Juba.

 Mwenyekiti wa chama cha SPLM ambaye pia ni Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ambacho Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihudhuria.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais wa Sudan ya Kusini Rais Salva Kiir mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu cha chama cha SPLM ,kikao hicho kilimalizika usiku wa manane mjini Juba ,Sudan.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati Kuu ya chama cha SPLM mjini Juba,kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SPLM ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo James Wani.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.