Habari za Punde

Wasanii na wajasiriamali wawasili wakitokea Oman


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi Khamis katikati akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar wa Abeid Karume akisubiri kuwasili kwa Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa Habari waliokuwa nchini Oman kwa ajili ya maonyesho ya Tamasha la Utamaduni yaliyofanyika nchini humo. (Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)




Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa Habari waliopata nafasi yakwenda Oman kwa ajili ya  kuutangaza Utamaduni wao wakipokelewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar. (Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)




Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi wa mwanzo kulia akiwasalimia wasanii hao baada ya kuwasili uwanjani hapo. (Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)






Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimuhoji mmoja kati ya Wasanii waliyopata bahati ya kwenda nchini Oman kwa ajili ya maonyesho hayo.
(Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)


Na Ali Issa Maelezo                                                             
Wasanii na Wajasiriamali kutoka Zanzibar waliokuwa wakishiriki Maonesho ya  Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Ujasiriamali yaliyokuwa yakifanyika nchini Oman hatimaye wamerudi Salama nchini.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Khamis Hamad ndio kiongozi wa Serikali aliyekuja kuwapokea baada ya kumaliza safari yao ya mwezi mmoja nchini humo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Uwanja wa ndege wa kimatifa wa Abeid Karume mara baada ya kuwasili Mkuu wa Msafara huo Khadija Battashy amesema safari ilikuwa na mafanikio makubwa sana kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kutokana na kuitangaza vyema nchi yao.
Amesema Wasanii hao waliweza kutumia vyema Vipaji vyao na kuweza kuwavutia Watazamaji na watu mbalimbali waliofika katika Maonesho hayo.
Bi Khadija ameongeza kuwa fursa ambayo waliipata ni muhimu na kwamba itaisadia Tanzania katika Sekta mbalimbali hasa biashara na Utalii.
Amesema wamebaini kuwa Biashara ya Viuongo inakubalika sana na kwamba Wajasiriamali walioenda kufanya bishara hiyo walifanikiwa vyema katika bishara yao.
Kuhusu biashara ya Mavazi Bikhadija amesema ilikuwa na changamoto kwao kutokana na Nguo walizopeleka kuwa Fupi jambo ambalo liliwapa shida kuuza nguo hizo.
Hata hivyo Bikhadija amesema Changamoto hiyo wataifanyia kazi na pale yatakapotokea Maonesho mengine Wataenda na Nguo ndefu ambazo zinapendwa sana kulingana na Utamaduni wa Watu wa Oman.
Kwa upande wa Sekta ya Utalii Bi Khadija amesema Wanamatarajio makubwa kwamba kiwango cha Watalii kinaweza kuongezeka kupitia Vivutio mbalimbali vilivyomo nchini walivyovionesha katika Maonesho hayo.
Ameongeza kuwa wapo Watu wengi kutoka nchi tofauti ambao wamevutiwa na hatimaye kujisajili kuja Tanzania kwa ajili ya Utalii katika Mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na Zanzibar.
Akizungumzia kuhusu Wasanii walioenda kutumbuiza katika Tamasha hilo Bi Khadija amesema kazi walioifanya ilikuwa ya kupigiwa mfano kutokana na Ngoma za Asili ya Zanzibar kuwavutia wengi katika Tamasha hilo.
Katika Msafara huo Jumla ya Watu 42 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar waliiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzani katika Maonesho hayo yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja ambapo nchi mbali mbali Duniani ziliweza kuonesha Vivutio na Kazi za Sanaa za Wananchi wake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.