Habari za Punde

JK ahudhuria mkutano wa kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini jijini Kigali, Rwanda

 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kwa furaha  sahada la maua baada ya kuwasili Kigali, Rwanda, tayari kwa mkutano  na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zilialikwa kuhudhuria mkutano huo. Mkutano huo ni ulijadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni leo Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.