Habari za Punde

Mahafali ya saba ya chuo cha utawala wa Umma

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiyapoke maandamano ya Wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar yaliyofanyika kwenye viunga vya chuo hicho kiliopo Tunguu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Utawala wa Umma wakionyesha furaha yao wakiwa katika mahafali ya kumalizia mafunzo yao ya cheti na Stashahada.

Wahitimu wa ngazi ya Stashahada wa Chuo cha Utawala wa Umma wakivaa kofia kuashiria kutunukiwa stashahada zao baada ya kuhitimu mafunzo yao hapo Tunguu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.



Mmoja wa wahitimu wa chuo cha Utawala wa Umma  waliofanya vyema kwenye mafunzo yao akikabidhiwa tuzo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif ambae ndie mgeni rasmi katika Mahafali ya saba ya Chuo hicho.

Balozi Seif akizungumza na wahitimu wa ngazi ya Cheti na Stashahada wa Chuo cha Utawala wa Umma kwenye mahafali ya saba ya chuo hicho hapo Tunguu.

Kushoto ya Balozi ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar Maalima Abdulla Suleiman, Mkurugenzi wa Chuo cha Utawala wa Umma Bibi Arusi Masheko Ali na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dr. Idriss Muslim Hijja.


Balozi Seif akikata Keki Maalum iliyotayarishwa na Wahitimu wa Chuo cha Utawala wa Umma kunogesha sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya chuo hicho vilivyopo Tunguu Wilaya ya Kati.

Picha na –OMPR – ZNZ.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.