TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA SHUGHULI ZA MKUTANO WA KUMI NA TISA WA
BARAZA LA NANE LA WAWAKILISHI UTAKAOANZA TAREHE 11 MACHI, 2015
Mkutano
wa Kumi na Tisa wa Baraza la Wawakilishi la Nane la Zanzibar unatarajiwa kuanza
kesho siku ya Jumatano tarehe 11 Machi, 2015, saa 3.00 kamili asubuhi.
Shughuli
za mkutano huo zitakuwa kama ifuatavyo:-
1.
Maswali na Majibu:
Maswali 77 yatajibiwa kwenye mkutano huu.
2.
Miswada ya Sheria:
Miswada Minne (4) ya Sheria itawasilishwa na
kujadiliwa,
Miswada yenyewe ni:-
(i) Mswada wa
Sheria ya Kuweka Masharti ya Usajili na Usimamizi wa Wathamini na Mambo Mengine
Yanayohusiana na Hayo.
(ii) Mswada wa
Sheria ya Kuanzisha Kamisheni ya Ardhi na Mambo Mengine Yanayohusiana na
Hayo.
(iii) Mswada wa
Sheria ya Kufuta Sheria ya Miradi ya Maridhiano Namba 1 ya 1999 na Kutunga
Sheria Mpya kwa ajili ya Kuanzishwa na kuendesha mashirikiano baina ya Sekta ya
Umma na Binafsi na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.
(iv) Mswada wa
Sheria ya Kuanzisha Baraza la Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar na Mambo
Mengine Yahayohusiana na Hayo.
3. Kuwasilisha mbele ya Baraza, Sheria ya
Kura ya Maoni Nam. 11 ya 2013 ya Jamhuri ya Muungano kwa Mujibu wa Kifungu
132(2) cha Katiba ya Zanzibar.
4. Taarifa za Serikali (Mawaziri)
kuhusu Utekelezaji wa Maagizo ya Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi
Mwaka 2013 /2014.
5. Ripoti za Kamati za Kudumu za
Baraza la Wawakilishi za Mwaka 2014/2015.
6. Taarifa ya Kamati Teule ya
Upotevu wa Nyaraka.
7. Hoja ya Mjumbe kuhusu
Ucheleweshaji wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
(Yahya Khamis Hamad)
KATIBU
BARAZA LA WAWAKILISHI,
10 Machi,
2015.
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment