WAZIRI wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati
wa Zanzibar, Mhe:Ramadhan Abdalla Shaaban akizungumza na wajumbe wa bunge la
Norway wakiongoza na mkuu wa msafara huo, Bwana Geir Hermansen, wakati
walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati
wa Zanzibar, Mhe:Ramadhan Abdalla Shaaban akisalimiana na mmoja wa wabunge wa
bunge la Norway katika eneo la VIP uwanja wa ndege wa Karume Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAJUMBE wa bunge la Norway wakiwa katika kikao
maalumu na viongozi wa Serikali ya Mikoa miwili ya Pemba, mkutano huo uliokuwa
ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mkoani
Mhe:Hemed Suleiman, mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Wilaya ya Mkoa Mhe:Hemed Suleiman Abdalla,
akizungumza na wajumbe wa bunge la Norway wakati walipowasili kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Msafara wabunge wa bunge la Norway Bwana
Geir Hermansen, akitoa salamu za wabunge wenzake kwa viongozi wa mikoa miwili
ya Pemba, huko katika ofisi ya Mkuu Wa Mkoa wa kusini Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MENEJA wa Shirika la Umeme zanzibar ZECO Mhe:Hassan
Ali Mbarouk, akiwasilisha Ripoti ya Umeme zanzibar uliofadhiliwa na Serikali ya
Norway, huko katika hoteli ya Pemba sunset Beach Wesha, huku wajumbe wa bunge
la Norway wakimsikiliza kwa makini Meneja huyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa wabunge wa bunge la Norway akiwasilisha
Ripoti ya Umeme, kwa viongozi wa Shirika la Umeme zanzibar ZECO,huko katika
hoteli ya Pemba Sunset Beach Wesha.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment