Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulraman Kinana akihutubia wakazi wa Itolwa wilayani Chemba mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara zake za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010.
Mawenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akiwahutubia wakazi wa Itolwa ambapo aliwaambia kuwa katika chaguzi za mwaka huu hatokata jina la chaguo la watu.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Itolwa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma ikiwa sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
Wananchi wakifuatilia hotuba za wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Kusini Juma Nkamia akiwahutubia wakazi wa Itolwa waliofurika kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa zinazohusu maji na umeme katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Chuki Galawa akiwasalimu wananchi wa Itolwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amepata mapokezi makubwa katika kijiji cha Chandama kata ya Mapango akiwa amaeongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa kusini Ndugu Juma Nkamia.
Wananchi wa kijiji cha Chandama wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrhamn Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Songolo
Wananchi wa kijiji cha Songolo wakimuimbia Katibu Mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman Kinana nyimbo za kumkaribisha katika wilaya ya Chemba.
Wananchi wa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua ,kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambapo katika kata ya Paranga alikagua maendeleo ya ujezi ya wodi ya mama na mtoto pamoja na kushiriki kupanda miti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika wodi ya Mama na Mtoto katika zahanati ya Kalema ,kata ya Paranga, wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Chemba.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu wilaya ya Chemba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Babayu mara baada ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya mtendaji.(Picha na Adam Mzee)
Kimsingi yeyote anaehoji uwezo wa CCM-Bara ktk kuleta umoja, maendeleo amani na utulivu lazima tuwe na wasi wasi na akili yake!
ReplyDeleteTatizo pekee la chama chetu liko zanzibar, kule mambo hayaendi kabisa viongozi wa chama hawafanyi kazi kabisa.
Visiwa vimechoka utadhani Tza inatawaliwa na vyama tofauti uzembe wa namna hii unaosababisha sisi huku kutumia nguvu nyingi kusaidia kutatua migogoro ya kisiasa visiwani badala ya kujitafutia maendeleo.
Kk mmevaa koti la muungano, lazima uongee hivyo, Zanzibar wana msimamo wao wa kisiasa, nawala huwezi kuwa zungumzia wa Zanzibar, ww huijuwi Zanzibar, ni bora ongelea unakokujua
DeleteKk mmevaa koto la muungano
ReplyDeleteKoti gani hilo la muungano tulilolivaa? wakati tunakusaidieni kwa kila kitu!.. kama tumevaa koti la muungano, vunjeni basi mfwe njaa au tukupeni kichapo!
ReplyDeleteNa wewe uliejibu hivo utakua CUF ndio mafedhuri na wamejaa tere huku Bara!