Habari za Punde

Mawakala wa EzyPesa Wakutana na Uongozi wa Zantel Zenj.

Mkurugenzi Masoko wa Zantel Zanzibar Ndg Mohammed Mussa Baucha akizungumza na Mawakala ya EzyPesa, katika ukumbi wa Bateiyamin Malindi Zanzibar, mkutano huo uliwahusisha mawakala wote  wa EzyPesa kuzungumzia Huduma ya Ezypesa kwa Wateja na jinsi ya uboreshaji wake katika kutowa huduma bora. 
Baadhi ya Mawakala wa EzyPesa Zanzibar wakifuatilia mkutano huo, katika ukumbi wa Bateyamin malindi Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Zantel Ndg Gabriel Kamukara, akizungumza katika mkutano huo na Mawakala wa EzyPesa kutokana huduma hiyo wanayotowa kwa Wateja wa EzyPesa. Na kuwataka mawakala wa EzyPesa kuwasiliana na Kitengo cha EzyPesa wakati wanapoona kuna matatizo ya kiufundi wanapokuwa katika huduma hiyo. 

Wakiwa Makini wakifuatilia mkutano huo na Viongozi wa Zantel.wakizungumzia huduma hiyo wanayotowa kwa wateja wao.


Meneja Muandamizi wa EzyPesa Ndg Leornad Kameta akijibu maswala yalioulizwa na Mawakala wa EzyPesa wakati wa mkutano huo 
Maofisa wa Zantel wakiwa makini kuchukua michango iliokuwa ikiwasilishwa na Mawakala wa EzyPesa. kujuwa matatizo wanayokabiliana nao wakati wakihudumia wateja wao wa EzyPesa.

                    Mawakala wamepata fursa ya kuuliza maswala kwa Viongozi wa Zantel


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.