Gwiji la Taarab asilia enzi zilee Msanii Khamis Juma akiwa miongoni mwa wabunifu na wasanii maalum wanne mwaka huu akikonga nyoyo za washiriki wa hafla ya zilizofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji Mirabaha ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh. Salim Nassor Ali –Jazeera akimkabidhi ngao mchangiaji bora wa kusaidia sherehe hizo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Mh. Salim Nassor – Jazeera akimkabidhi ngao msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ustaadhi Suleiman Haji Suleiman akipokea kwa niaba ya Mhe. Balozi Seif ambae Ofisi yake imegharamia sherehe hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati akimkabidhi ngao Msanii Khamis Juma baada ya kufuzu kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.
Al - Anisa Mwapombe Hiari tetere wa nyimbo za Taarabu aliyevuma ndani ya mwambao wa Afrika katika miaka ile akifurahia zawadi ya ngao na fedha taslim alizokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.
Msanii wa Kizazi kipya Baby Jay akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Berry Black Kijana wa Muziki wa Kizazi kipya akichekelea na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya ugawaji Mirabaha pamoja na washindi mbali mbali wa tuzo za wabunifu na wasanii bora kwa mwaka huu mara baada ya kukamilika jkwa sherehe hizo hapo Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis,Msanii Khamis Juma, Msanii Mwapombe Hiari na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali M,barouk, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi, Mjumbe wa Kamati ya Ugawaji Mirabaha Mh. WEanu Hafidh Ameir pamoja na Mchangiaji bora wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Mahadh Juma Maalim.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment