Familia zisizopungua 200 zimeathirika baada ya kukumbwa na mafuriko ya mvua huko Zanzibar,
Zanzibar Diaspora Association inakusanya michango ili kusaidia ndugu jamaa na marafiki waliokumbwa na majanga hayo, kwa yoyote anaetaka kuchangia awasiiliane na Mwenyekiti wa ZADIA Bwana Omar Ali Sim Mumbari ya simu, 1 (215) 459‑4449
Unaweza kuchangia Online kupitia
Karibu kusikiliza Mahojiano yetu na Mwenyeji wa Zanzibar akielezea maafa ya mvua za masika
Maafa yametokea tumshukuru Mungu, lakini hii hoja ya kuwalaumu wananchi eti wamejenga mabondeni ni ya kipuuzi. Serikali imefanya nini hasa katika suala la kuwapatiaw wananchi wanyonge viwanja vilivyopimwa katika maeneo stakihi kujengwa majumba. Kila ikitokea kutolewa viwanjwa vilivyopimwa basi wanaopewa ni hao hao wakubwa wa nchi, wafanya biashara wakubwa basi. Hivi unafikiri mnyonge ajenge wapi?? Kila siku tunalaumu tuu wananchi lakini ukweli unabaki palepale serikali zetu bado hajidhamiria kutatua kero hasa za wananchi.
ReplyDeleteSuala jengine ni kukosekana mipango miji thabiti hapa Zanzibar. Mzungumzaji amesema watu wamejenga kwenye maeneo yaliyokuwa yanapita maji hapo zamani na hivyo kupelekea kuziba kwa mitaro. Hili ni sawa kwa upande mmoja. Lakini nitoe mfano mmoja, tumeona hapo kwenye picha eneo la mbele la Airport ya Zanzzibar na barabara ya Kiembesamaki ambayo wageni wote wanaoshuka ndege Zanzibar wanapita hapo pamejaa maji (pamefurika kabisa) pale ni suala la kukosa mipango sahihi. Hakuna mitaro ya maji kaatika barabara nyingi hapa Zanzibar pamoja na mitaani, ka kweli Zanzibar hakuna kabisa eneo unaloweza kusema at least liko 'semi-planned' si Mbweni si Chukwani si Mombasa almudadi ni vurugu mechi. Hatuna Mji hasa unaoeleweka kama huu ni mji hasa. Ikinyesha mvua kidogo tu barabara zote hazipitiki.
Wanasiasa wapo kutunisha matumbo yao tuu wanashindwa kabisa kuibana serikali kaatika mambo ya msingi kabisa. Imagine pale Mwanakwerekwe, lile tatizo lipo kwa miaka mingi sana, lile ni Jimbo la aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali kwa Miaka kumi (Mh. Shamsi Vuai Nahodha) alikuwa na influence kubwa ya kutengeneza ile sehemu akiwa ni Mwakilishi wa Jimbo lakini pia kama second person kwa ukubwa wa nchi kwa miaka kumi. Hakuna lolote. Leo njia ya kutoka sokoni M/Kwerekwe kuelekea Fuoni haipitiki kabisa badala yake tunatumia vijia vya vichochoroni kabisa ili kuipata Fuoni na m aeneo jirani na huko. Serikali, wanasiasa kwa miaka yote wanaliona hili lakiji kimyaa kabisa (mkono unakwenda vizuri kinywani basi, huku wananchi wanateseka).
Viongozi eleweni kwamba uongozi ni dhamana na mtaulizwa huko tunakokwenda. Ondosheni shida za wananchi.