Habari za Punde

Mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania JET

 WANACHAMA wa chama cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania JET, wakifuatilia ripoti ya utendaji kazi kwa mwaka uliopita, kwenye mkutano mkuu ulioambatana na uchaguzi, uliofanyika juzi hoteli ya Lion Sinza jijini Dar-es Salaam, (Picha na Haji Nassor, Dar-es Salaam).
 MKURUGENZI mtendaji wa chama cha waandishi wa habari Tanzania JET, John Chikomo akijibu hoja za wajumbe wa mkutano mkuu wa JET, ulioambatana na uchaguzi mkuu, kulia ni Mwenyekiti wa kikao hicho Aish Dachi, mkutano huo ulifanyika hoteli ya Lion Sinza, (Picha na Haji Nassor, Dar-es Salaam).
MWENYEKITI mpya wa JET Dk, Helen Otaro akitoa neno la shukuran kwa niaba ya viongozi wake wapya, baada ya kuchaguliwa kwenye mkutano mkuu ulioambatana na uchaguzi, uliofanyika hoteli ya Lion Sinza jijini Dar-es Salaam, kulia ni Makamu Mwenyekiti Ali Haji Hamad, na kushoto ni Mkurugenzi mtendaji John Chikomo, (Picha na Haji Nassor, Dar-es Salaam).  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.