Habari za Punde

Matokeo ya Kura ya Maoni ya Wagombea wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja

Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja Fatma Shomar Omar akitangaza matokeo ya majimbo matatu ya Kikwajuni, Jangombe na Malindi Jimbo la Kwahani matokeo yake bado kukamilika kwa baadhi ya vituo na kutolewa baadae leo mchana, wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika Afisini kwake Miti Ulaya Unguja mchana huu.

Jimbo la Kikwajuni waliojitokeza kugombea Ubunge walikuwa Wanachama 6. Mshindi wa kwanza wa Kura ya Maoni katika Jimbo hilo kwa
Nafasi ya Ubunge Eng Hamad Yussuf Masauni, ametetea vizuri kiti chake na kurudi tena katika Jimbo hilo,kwa kupata kura 2,222
Mshindi wa Pili Ndg Mussa Shaali Chum aliyepata Kura 461,
Mshindi wa Tatu Mwanamama Nuru Mohammed Ahmed aliyepata kura 155,
 wengine waliogombea jimbo hilo
 Nafasi ya 4 imechukuliwa na Ndg Abdulkadir Abdurazak Mukrim amepata Kura 146
Nafasi ya 5 Ndg Parmukh Singh Hoosan kura 78, Nafasi ya
6 Ndg Eng Nassiri Ali Juma kura 74,

Kwa Nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Kikwajuni aliyeibuka kidedea ni aliyekuwa Mwakilishi wa Rahaleo Mhe Nassor Salim Ali Jazira,kwa ushindi wa kura 1200

Nafasi ya Pili imechukuliwa na Ndg Mohammed Ali Ahmed (Kibahola) kwa kupata kura 818.

Nafasi ya Tatu imechukuliwa na aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Mahmoud Mohammed Mussa kwa kupata kura 529.

Nafasi ya Nne imechukuliwa na Ndg Saleh Ali Abdallah kwa kupata kura 305

Nafasi ya tano imeshikwa na Ndg Khatib M Khatib (Tido) kwa kupata kura 122.

Nafasi ya sita imeshikwa na Ndg Said Shaban Said kwa kupata kura 90

Na nafasi ya mwisho ya kinyang'anyiro hicho imechukuliwa na Ndg Ibrahim Ali Said kwa kupata kura 86. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.