Habari za Punde

Kongamano la kujadili mwenendo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015


 Baloz Ali Karume akizungumzia Muungano wa Tanzania na Mamlaka kamili ya Zanzibar kwenye Kongamano la kujadili mwenendo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 na umuhimu wake katika kujenga Zanzibar,  Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa  Grand Palace Mjini Zanzibar.
 Balozi Amina Salum Ali akizungumzia umuhimu wa Ilani  ya Uchaguzi  Mkuu ya 2015 ya CCM katika Kongamano la kujadili mwenendo wa kampeni za Uchaguzi na umuhimu wake katika kujenga Zanzibar lililofanyika Ukumbi wa  Grand Palace Mjini Zanzibar.
 Mshiriki wa Kongamano hilo Rashid Kheri akitoa mchango kuhusiana na Muungano wa  Tanzania na Mamlaka  ya Zanzibar kwenye Kongamano lililo fanyika Grand Palace Mjini Zanzibar.
 Mwanaharakati kutoka Jumuiya ya Mikunguni Youth Development Organisation (MYDO) Zahra Yahya Rashid akitoa mchango wa umuhimu wa kuwa na Ilani katika Uchaguzi kwenye Kongamano  hilo.
 Mwenyekiti wa Kongamano Mahmoud Thabit Kombo akifafanua masuala mbali  mbali yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015 kwenye Kongamano la kujadili mwenendo wa kampeni za Uchaguzi 2015 na umuhimu wake katika kujenga Zanzibar  katika Ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar

Wanachi mbalimbali wakisikiliza kwa umakini kongamano hilo.
PICHA NA ABDALLA OMAR-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.