Habari za Punde

Kundemba yaanza vyema ligi daraja la pili yaifunga Rascazone 3-2

Timu ya Kundemba FC leo imeanza mechi yake ya kwanza kwa ushindi wa magoli 3-2 katika ligi ya Daraja la Pili.

Kundemba ilicheza na timu ya Ras Cazone katika uwanja wa Amaan ambao ulianza saa 8:00 mchana.

Magoli ya Kundemba yalifungwa na Sadi Mgeni ambae kwa leo alikua captain yeye aweka kimiani magoli 2 yote kwa njia ya penalti.

Goli la 3 lilifungwa na Ali Abdalla almaarufu 'dume' mnamo dakika za 85 ambaye alitokea bench.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.