Habari za Punde

Mama Mwenamwema Shein, Awataka Wanawake Kumchagua Dk Shein na Dk Magufuli.

Katibu wa UWT Wilaya ya Kaskazini B Unguja Bi. Khabija akisoma risala ya Wanawake wa UWT, wakati wa mkutano wao na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbin wa afisi za Jimbo la Kitope kinduni. 
 Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akipokea risala ya Viongozi wa UWT wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja, kutoka kwa Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo Bi Khadija.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Muaasisi wa Umoja wa Wanawake Zanzibar Mama Fatma Karume akiwahutubia Wanawake wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja na kuwata kuipigia kura CCM wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Afisi za Jimbo la Kitope Kinduni Zanzibar.

Mama Fatma Karume akisisitiza jambo wakati akitowa historia ya Zanzibar juu ya Wanawake wakati huo wa enzi za zamani mwanamke alikuwa hapigi kura na kuwata Wanawake kutumia fursa hii kuipigia kura CCM na kumchagua Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Magufuli.
Umoja wa Wake wa Viongozi wa CCM Zanzibar Wabunge na Wawakilishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano katika Afisi za Jimbo la Kitope wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza nao na kumuombea kura Dk Shein. na Wagombea wote wa CCM.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati wa mkutano na Mama Mwanamwema Shein. na kuwataka kuichagua CCM ili kuzi kuleta maendeleo kwa Wazanzibar na kudumisha Amani Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wanawake wa Wilaya ya Kaskazini Unguja wakati wa ziara yake na kuwatajka kuwapigia kura Wagombea wa CCM katika uchaguzi Mkuu na Mkumpigia Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati alipokutana na Viongozi wa Umoja wa Wanawake wa UWT na kumuombea kuwaombea Kura Wagombea wa CCM kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyikia mwishoni mwa wiki hii. 
Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibarv Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia katika ukumbi wa Afisi za Jimbo la Kitope Unguja, akiwa katika ziara yake ya kuwaombea kura wagombea wa CCM kwa Viongozi wa UWT wa Mkoa huo.  

Vijana wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakishangilia wakati wa mkutano wa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein kuwaombea kura wagombea wa CCM, katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Imetayarisha na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
Mob. 0777 424152 or 0715424152.
Email. othmanmaulid@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.