MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada ya umuhimu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu, kwenye mdahalo ulioandaliwa na asasi ya kirais ‘PACSO’ kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo, Ali Said Hamad na kushoto ni Mwenyekiti wake Omar Ali Omar, mdahalo huo umefanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
MWANACHAMA wa Jumuia ya wanawake
wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAUZA’ Hidaya Mjaka Ali, akichangia mada kwenye
mdahalo wa jukwaa la amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu, mdahalo huo,
umeandaliwa na asasi ya kiraia ‘PACSO’ Pemba, na kufanyika skuli ya sekondari
ya Fidel Castro, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
Wasema ‘Foundation’
hawakukosea kuiwezesha asasi hiyo
Na Haji Nassor, Pemba
Wamejisifia
kuwa, wanasiasa wamekuwa wakiwachanganya juu ya amani, maana wapo wengine
wamekuwa wakitoa maneno ya vijembe wakati wakinadi sera zao.
Wapiga
kura hawa kutoka wilaya za Chake chake na Mkoani, wamejigamba kuwa sasa, wameshapata
uwelewa mkubwa kupitia midahalo ya PACSO.
Wakati
wakimuhadisia mwandishi wa makala haya, kutaka kujua ni nani aliwaita kwenye
midahalo hiyo, walisema kuwa ni Mmwevuli wa Mtandao wa Asasi za kiraia Kisiwani
Pemba, ‘PACSO.
Wakizungumza
nami wananchi hawa wanasema ‘PACSO’ midahalo hiyo imewaweka wazi kwani hapo
awali walikuwa wakibabaishwa na wanasiasa.
Uwelewa
walioupata, kupitia midahalo hiyo, imeweza kuwasaidia sana maana kwa sasa wanachofanya
ni kuhakikisha wanakatazana vile viashirio vyote vya uvujifu wa amani.
Akizungumza
kwenye mdahalo uliofanyika Skuli ya
sekondari ya Fidel csatro wilaya ya Chake chake Omar Khamis Ameir wa Chake
chake anasema suala la maelekezo ya wanasiasa kulinda kura halikuwa na tija.
“Kumbe
hata kulinda kura, kwa maana ya kukaa mita 200, ni jambo ambalo linaweza kuzaa
matunda mabaya, lakini haya nimeyafahamu kwenye mdahalo wa ‘PACSO’ alisema.
Asha
Haji Makame, nae anasema kuwa kabla ya kushiriki katika mdahalo huo, hakuwa na
uwelewa mpana wa jinsi nafasi yake ya kulinda amani na utulivu.
“Mimi
kupitia mdahalo huo, ndio nimepata uelewa kumbe kila mwananchi anayonafasi ya
kufanikisha uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu, maana moja ni kuwaelimisha
wengine’’,alieleza.
Nae
Juma Kombo Hassan wa Jimbo la Wawi wilaya ya Chake chake alielezea kupata
taaluma kubwa juu ya kutunza amani na umuhimu wake.
Mwanajuma
Haji Mmaka, wa Mkoani anasema midahalo kama hiyo ingefaa sana kufanyika hata
kabla ya kuanza kwa kampeni.
“Mimi
naona midahalo kama hii ya jukwaa la amani wakati na baada ya uchaguzi,
ingefanyia kabla ya kuanza kwa kampeni ili sisi wananchi tupate elimu pana’’,alifafanua.
Katika midahalo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji
wa ‘PACSO’ Ali Said Hamad, yeye anasema kila mmoja anayo nafasi ya
kuufanikisha uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.
Mkurugenzi
huyo, anasema mwandishi wa habari, wanasiasa, wapiga kura, wanawake, watu wenye
ulemavu na vijana wanaweza kutuliza mizuka yao na amani iliopo ikadumu.
“Mimi
naamini kwa hizi wilaya mbili tulizozifikia na wananchi kushiriki vyema, basi fedha za ‘Foundation for Civill Society’
hazikutumika bure, maana hata wananchi walihamasika juu ya umuhimu wa kutunza
amani’’, alibainisha Mkurugenzi huyo wa PACSO.
Kwa
ujumla wananchi zaidi ya 500 ndani ya mkoa wa kusini Pemba ambao inaumndwa na
majimbo tisa, walifikiwa na taaluma hiyo kupitia midahalo ya wazi na kuibua
changamoto kadhaa na kupelekea uchaguzi kuwa wa amani.
Kwa
mujibu wa andiko la mradi, walengwa walikuwa ni 230, ingawa kutokana na
wananchi kuhamasika na kuona kuwa kwenye asasi hiyo ndiko watapata taaluma,
walivuuka lengi na kufikia 500.
“Wananchi
wengine wamekuja hata wakualikwa, waliposikia tu kuwa mdahalo wa amani
walikuja, tulipowaliuza walisema kwenye vyama vyao hubaniwa taaluma hiyo”,
alisema Makamu Mwneyekiti wa PACSO Aisha Abdalla Rashid.
Hakusita
kusema inaonyesha wananchi walikuwa na hamu na midahalo ya asasi ya kirai, na
hasa kutokana na kutoegemea upande mmoja wa chama wala serikali.
Hata
hivyo ameiomba ‘Foundation for Civil Society’ ya Da –es Salaam kuendelea kuwawezesha
kila muda ili Tanzania iwe na wananchi wanaofahamu wajibu na haki zao katika kulinda
amani na utulivu.
Mwenyekiti
wa PACSO, Omar Ali Omar anasema miongoni mwa makundi yaliofaidika na midahalo
hiyo ni viongozi wa dini, wanawake, wenye ulemavu, vijana pamoja na wanasiasa.
“Unuaju
kila mmoja anafahamu athari na faida za amani, lakini kwa makusudi ‘PACSO’
imeamua kuusaka mradi huu ili kukumbushana’’,alifafanua.
Akiwasilisha
mada kwenye mdahalo uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel castro, Mratibu wa
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, Fatma Khamis Hemed, alisema suala la
amani ni tunu ya taifa.
Anasema
kama hivyo ndivyo, ni vyema kila mwananchi kuona ananafasi ya kutunza amani na
utulivu uliopo, ili taifa libakie kwenye hali hii hata baada ya uchaguzi.
“Jamani
amani haichezewi, amani haijaribiwi kuvunjwa na wala haina mbadala wake, sasa
lazima tuitunzeni sana ‘’,alisisitiza.
Mwanaharakati
wa kijamii Abubakar Mohamed Ali, akiwasilisha mada ya umuhimu wa amani, kwenye
ukumbi wa ZAYEDESA Mkoani Pemba, alisema wanaotaka kuvunja amani waangali nchi
jirani.
Yeye
anasema PACSO, imepata mradi huo wakati mwafaka maana, kila mmojana anadhani
suala la kuhimizana amani na utuli kama vile ni kazi ya vyombo vya ulinzi na
usalama pakee.
“Lazima
suala la kutunza amani na utulivu, tusilipe kipaumbele tu hata baada ya
uchaguzi kumalizika, lakini hata baadae maana Tanzania ipo’’,alisema.
Yeye
aliipongeza sana PACSO, kutokana na kuona umuhimu wa kuwa na mradi huo ambao,
ndio uliotoa dira na mwanga kwa jamii, maana wanasiasa wamekuwa wakiwachanganya
wapiga kura wao.
Ingawa
Makamu Mwenyekiti wa PACSO, Aisha Abdalla Rashid, yeye anasema kama kweli jamii
ikiyaapuza maelekezo yasio na tija ya wanasiasa, basi amani ya kudumu
itapatikana.
“Wapo
wanasiasa wameku wakitoa lugha za viashirio vya uvunjifu wa amani, na wapo
wananchi wamekuwa wakiunga mkono, sasa hilo sio jambo jema’’,alifafanua.
Baadhi
ya wananchi waliipongeza PACSO kutokana na uamuzi wake wa kuingilia kati, suala
la kutoa elimu ya umuhimu wa amani, na hasa kwa vile vyama vimekuwa vikitoa
elimu ambayo ndani yake inawakalakini.
Kwenye
mafanikio, basi huwa na changamoto hazikai mbali, maana PACSO nayo ilikumbana
nazo, ikiwa ni pamoja na mradi huo kuja wakati tayari kampeni zimeshawiva.
Jengine
ni kukosekana hasa kwa wale wagombea husika kwa maana ya wabunge na
wawakilishi, maana wengi wao walishajipangia ratiba za mikutano ya kampeni.
Ilionekana
ilikuwa vigumu kwa kundi moja wapo la walengwa hao, kuhudhuria wao wenyewe
kwenye midahalo ya PACSO, kutokana na kutingwa na safari ya kusaka kura.
“Kila
kitu fedha, na fedha ikiwa kidogo huwezi kufanya kitu, nasi fedha shilingi 15
milioni zilikuwa hazitoshi, kama the foundation wengietupa alau shilingi 45
milioni basi twengefanya kila kitu’’,alifafanua Sifuni Ali Haji.
Yeye
ameiomba foundation wakati mwengine kuwapatia fedha zenye kiwango kikubwa na
kupewa walau mwezi mmoja kabla ya kampeni, ili kuhakikisha wanafikia walengwa
wote.
Mmwevuli
wa Mtandao wa Asasi za kiraia Kisiwani Pemba (PACSO), ambao umeanzishwa mwaka
2006 na unao wanachama 76 asasi za kiraia na umeshawahi kupatiwa ufadhili
miradi mitano na Foundation ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka 2008 wa kuwajengea
uwezo, Midahalo ya rais pamoja na mdahalo wa mchakato wa katiba.
No comments:
Post a Comment